Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt Suleiman Jafo akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo cha mafuta cha Oryx kilichopo Mwenge ambacho kinatumia Nishati mbadala leo Ijumaa Februari 24, 2023 jijii Dar es Salaam, anayepiga makofi ni Mkurugenzi Mtendaji wa Oryx Energies Tanzania Limited Kalpesh Mehta.
Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt Suleiman Jafo akizungumza kabla ya kufanya uzinduzi wa kituo hicho cha mafuta kinachotumia nishati mbadala.
Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt Suleiman Jafo akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Oryx Energies Tanzania Limited Kalpesh Mehta alipokuwa akitoa maelezo kabla ya kufanya uzinduzi wa kituo hicho.
Picha ya pamoja.
Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt Suleiman Jafo amewataka watanzania kupendelea kutumia Nishati mbadala ili kupunguza uzalishaji wa Hewa na changamoto ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi.
…………………………………….
Waziri Dkt Jafo ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam wakati akifungua kituo cha Oryx Mwenge kinachotumia umeme wa jua Sollah Power ambapo amesema pindi matumizi ya gesi yanapoongezeka Nchini yanasaidia suala la utunzaji wa mazingira.
Aidha Waziri Dkt Jafo ameyasisitiza makampuni yanayozalisha mitungi hiyo kuangalia taratibu za kuwakopesha watanzania ili kuwasaidia wananchi kuweza kuitunza nchi kwa kiwango kikubwa
“Serikali itahakikisha inatoa maelekezo Kwa Taasisi zote zinazotumia kuni na mkaa Kwa kiwango kikubwa kutumia Nishati mbadala ili kuweza kuikomboa nchi chetu”amesema Dkt JAFO
Ameeleza kuwa malengo ya nchi wanatarajia kupunguza kati ya Asilimia 30-35 ilifika Mwaka wa 2030 hivyo ameyataka makampuni mengine kuiga mfano wa Oryx.
Amesema katika kujali mazingira jukumu lake ni kuhakikisha wanapambana na changamoto ya mabadiliko ya Tabia nchi lakini pia kuyafanya Mazingira yawe salama.
Waziri Dk.Jafo amesema kuwa katika maendeleo endelevu lengo la saba la malengo ya milenia linasema tutumie nishati za kisasa kwa ajili ya kuzalisha nishati mbalimbali , hivyo Oryx Energies wameamua kulifanya hilo huku akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Oryx Energes Kalpesh Mehta kwani ameamua kujipambanua .
Aidha amesema Oryx Energies imekuwa mfano wa kuigwa na hiyo imejionesha kwenye maelezo yao kuwa wanazalisha KWh 21 na matumizi yao ni KW tisa , hivyo malengo yao ni kupeleka ziada ya umeme wanayozalisha kwa kutumia Solar energies katika gridi ya Taifa.
Ametumia fursa hiyo kuziomba kampuni nyingine zote za mafuta kama zitaiga mfano mzuri wa Oryx Energies wa kutumia nishati mbadala sababu watapunguza athari za mabadiliko ya tabianchi.“Kuja na mfumo wa kutumia umeme wa jua ni kuunga mkono juhudi za Serikali za kupunguza hewa ukaa ambapo pia huo ndio mkakati za Serikali inayoongozwa na Rais Dk.Samia.”
Amesema katika malengo endelevu ya kidunia lengo la Saba linalosema itumike Nishati za kisasa Kwa ajili ya kuzalisha Nishati mbalimbali Kampuni hiyo kwa kufanya uwekezaji utakaolinufaisha Taifa.
Pia Waziri Huyo ametumia fursa hiyo kuwataka watanzania kuwaunga mkono wawekezaji wanaounga mkono maono za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ili waweze kufanikisha malengo mbalimbali waliyojiwekea katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Oryx Energies Tanzania Limited Kalpesh Mehta amesema wanayo furaha kwa kituo cha Mwenge jijini Dar es Salaam kimeanza kutumia nishati ya umeme wa jua(Solar Power) na kwamba hiyo ni hatua ya kwanza kwani watakwenda hatua 10 zaidi kwa nchi nzima kwenye vituo vyao vya mafuta pamoja na maghala ya kuhifadhi mafuta ambako watatumia ishati ya umeme wa jua.
“Hivyo tumefurahi kuja kwa Waziri Dkt.Jafo na amesema mameno mazuri ambayo yametupa nguvu ya kuendelea kufanya vitu vingi na mwaka huu na mwaka ujao tutafanya kazi nyingi na tuhakikisha vituo vyote vinatumia umeme wa jua .Tumeamua kutumia Solar kwani itasaidia kupunguza gharama kubwa, hivyo mikakati yetu ni kutumia umeme jua katika vituo vyetu vyote pamoja na maghala yetu ya kuhifadhia mafuta .”
Aidha amesema Wahandisi wao wamefanya kazi nzuri kwa kuweka mfumo mzuri wa kuhakikisha mfumo wa Solar energy unatumika saa 24 na kuhusu mipango ya Oryx Energies kuweka vituo vya kujaza gesi kwenye magari amesema ni jambo ambalo wanalifanyia kazi kwa kuzungumza na wadau mbalimbali wakiwemo wanaoweza kuweka mifumo ya mabomba ya gesi.