Katika Maadhimisho ya PEPFAR Jijini Washington DC, Marekani, Rais Mstaafu Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na Watanzania Mama Tatu Msangi na Bintiye Faith Mang’ehe. Mama Tatu Msangi anaishi na virusi vinavyosababisha UKIMWI kwa zaidi ya miaka 17 sasa. Binti yake Faith alizaliwa bila virusi hivyo japo Mama yake alikuwa na virusi tangu Faith akiwa tumboni. Mama Tatu na bintiye Faith ni kielelezo cha mafanikio ya kuzuia maambukizi ya Mama aliyeathirika kwa mtoto akiwa tumboni na wakati wa kunyonyesha. Faith ana umri wa miaka 17 sasa.