…………………….
NA MUSSA KHALID
Shirika lisilokuwa la kiserikali la shahidi wa Maji -SwM limewakumbusha watanzania kuchangia utunzaji na rasililimali za vyanzo vya maji ili kusaidia kuepukana na changamoto ya ukosefu wa Maji katika maeneo mbalimbali nchini.
Kauli hiyo imetolewa Leo mkoani Morogoro na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika Hilo Abel Dugange wakati akifungua Warsha ya Mafunzo kuhusu Program ya kupaza Sauti ambayo imewakutanisha wadau kutoka katika taasisi mbalimbali nchini.
Aidha Dugange amesema kuwa sekta yeyote ile ni lazima kuwe na maji kwani ni salama kwa nchi kutokana na Mazingira mengi huwa yanategemea maji.
“Dhamira yetu ni kuangalia namna wadau wanaweza kushirikiana nasi katika kuhakikisha wanapaza Sauti ya changamoto ya upatikanaji wa Maji katika maeneo yao”amesema Dugange
Mkurugenzi Huyo amesema kila mwananchi anawajibu wa kutunza vyanzo vya maji kwani anayohaki ya kupata maji salama na kwa kiwango kinachotakiwa katika vizazi vya Sasa na vijavyo.
Amesema wanashirikiana na waandishi wa habari Ili kuangalia namna wanaweza kufikisha elimu kwa jamii kuhusu changamoto ya uharibifu wa vyanzo vya maji.
Kwa Upande wake Meneja Program Shahidi wa Maji Pendo Yera akieleza kuhusu program ya uhakika wa maji amesema kuwa baadhi wananchi wamekuwa wakisababisha changamoto hiyo.
Amesema kuwa Shirika Hilo linatumia mbinu ya kufanya ushawishi kwa kushirikiana na Jamii husika kuona namna ambavyo watazitatua changamoto hizo kwa kuwapatia elimu kuhusiana na haki na wajibu wao.
Naye Afisa Program kutoka Mashahidi wa MAJI John Muma amewasilisha mada kuhusu Hali na wajibu wa raia katika usimamizi wa rasilimali za maji ambapo ameeleza umuhimu wa usimamizi wa Pamoja kuwa dhana hiyo ni Muhimu kwa sababu maji ni muhimu kwa Maisha ya viumbe vyote.
“Katika usimamizi rasilimali za maji sera ya maji (2022) na sheria ya Usimamizi wa rasilimali za maji Namba 11 ya Mwaka 2008 zipo Ng’anzi tano ikiwemo ngazi ya Taifa,ngazi ya mabonde,ngazi ya Wilaya na ngazi ya Jamii ama jumuiya za watumia maji”amesema Muma
Kibwana Kia Shahidi wa Maji kutoka kata ya Tungi amesema katika kata yao kumekuwa na changamoto upatikanaji wa Maji jambo ambalo limesababisha wananchi kutumia Mani ambayo sio salama.
Miradi Hawaji Simba Shahidi wa Maji kutoka Kigogo Dar es salaam katika bonde la msimbazi amesema wamekuwa wakipambana na watu ambao wanahusika kufanya uharibifu wa moto kwa kutiririsha maji taka na hivyo kuharibu vyanzo vya maji.
“Kuhusu Mazingira ya utoaji wa taka ngumu kutokana na uhaba wa magari ya Manispaa kuwa haba mateja wamekuwa wakichukua katika majumba ya watu na kwenda kutupa taka kwenye mto”amesema Simba