Mwenyekiti wa Chama Cha waandishi wa habari Mkoa wa Mwanza (MPC), Edwin Soko, ameliomba Bunge la Jamuhri ya Muungano wa Tanzania kukubali mabadiliko mengine ambayo hayakusomwa Bungeni Februari 10, mwaka huu wakati wa kuwasilisha mswada wa mabadiliko ya sheria ya Huduma za habari.
Ombi hilo amelitoa leo Februari 19,2023 alipokuwa akizungumza wakati akitoa maoni yake juu ya kusomwa kwa muswada huo uliosomwa hivi karibuni.
Soko ameeleza kuwa matarajio yake kwenye mabadiliko ya sheria hiyo siyo makubwa sana kutokana na mambo yaliyopelekwa Bungeni siyo matatizo yanayoikumba sekta ya habari.
” Kunamambo mengine pia ambayo yalitakiwa kupelekwa Bungeni na kufanyiwa marekebisho ikiwemo yaliyopendekezwa kama vile maslahi kwa waandishi wa habari,ulinzi na usalama pindi wawapo kazini” amesema Edwin Soko.
Amewaomba wabunge wa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tazania kuhakikisha wanachangia vizuri muswaadahuo mara utakapoana kujadiliwa hapo baadaye na hatimaye upitishwe na kuwa sheria.
Ameongezakuwa ltakuwa jambo zui utakapopitiswa muswaada huo nakuwa shreria kwa sababu nina imani waandishi wa habari watafanya kazi wauhuru na weledi zaidi ili kuipatia jamii habari iliobora na zenye viwango.