KAMPUNI ya Kemmon Sports Agency imesema mabondia nguli wa Tanzania Seleman Kidunda watapanda ulingoni Februari 24 mwaka huu katika pambano la kimataifa litakalofanyika kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza jinini Dar es salaam.
Promota na Mkurugenzi wa Kemmon Agency Saada Kasonso amesema pambano litakuwa la ubingwa na litahusisha mikanda mitatu.
Kasonso amesema Kidunda atazichapa na Patrick Mukala raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo anayeishi nchini Afrika Kusini wakiwania ubingwa wa ‘ABU’ uzito wa Super Middle.
“Wakati Tony atapambana kuutetea ubingwa wake wa ‘ABU’ uzito wa Super Bantam, dhidi ya Sabelo Ngebinyana kutoka Afrika Kusini,” amesema Promota Kasonso.
Aidha amesema kutakuwa pia na pambano la ubingwa wa TPBRC.
Promota Kasonso ameeleza kwamba mbali na mapambano hayo kutakuwa na mapambano ya utangulizi.
Amebainisha kuwa lengo la kuandaa mapambano hayo ni kuwapa hamasa vijana wanaoshiriki mchezo wa ngumi nchini.
“Lakini vile vile tunawapa uthamani mabondia wetu,” amesema.
Ameeleza kwamba mapambano hayo yatakuwa ni yakukata na shoka kwani mambondia wote ni wauhakika na sio wa mchongo.
Amesema kwamba hadi kufikia siku ya mapambano mabondia wote watakuwa wameshalipwa fedha zao.
Kwa upande wake Tony amesema kwamba amejiandaa vizuri kwa pambano lake na atahakikisha anashinda ili kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania.