Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro mwenye suti ya bluu ,Naibu Waziri Wizara ya Katiba na Sheria Geophrey Pinda mwenye suti nyeusi, Lulu Ngw’anakilala kutoka LSF wa kwanza kulia na, Mansura Kassim Katibu Mkuu Wizara ya Katiba, Sheria na Utawala Bora Zanzibar Zanzibar wakizindua kitabu cha muongozo wa Kampeni ya Kitaifa ya Huduma ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia. Uzinduzi huo wa kampeni hiyo umefanyika leo Februari 15, 2023 jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro mwenye suti ya bluu, Naibu Waziri Wizara ya Katiba na Sheria Geophrey Pinda mwenye suti nyeusi, Lulu Ngw’anakilala kutoka LSF wa kwanza kulia na, Mansura Kassim Katibu Mkuu Wizara ya Katiba, Sheria na Utawala Bora Zanzibar Zanzibar wakiwa wameshika kitabu cha muongozo wa Kampeni ya Kitaifa ya Huduma ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia. Uzinduzi huo wa kampeni hiyo umefanyika leo Februari 15, 2023 jijini Dar es Salaam.
…………………………..
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro amezindua Kampeni ya Kitaifa ya Huduma ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia.
Amesema ili kutekeleza hayo yote Serikali itashirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo asasi za kiraia ambao watajengewa uwezo katika kutekeleza jukumu hilo.
Pia Waziri Ndumbaro ametoa wito kwa wananchi na wadau kushirikiana na wizara katika kampeni hiyo kwa kutoa taarifa sahihi na kwa wakati ili kuhamasisha utii wa sheria, kutoa elimu sahihi kwa umma, kutoa unasihi kwa waathirika wa ukatili, kutoa ushirikiano kwa vyombo vya utoaji haki, kutoshiriki matukio ya uvunjifu wa sheria,kuwalinda watoto katika maeneo yote (nyumbani, shuleni, njiani, kwenye vyombo vya usafiri na kwa njia nyingine zitakazoonekana zinafaa.
Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Legal Services Facility (LSF), Lulu Ng’wanakilala, amesema taasisi yake itaendelea kushirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria ili kuhakikisha kampeni hiyo inafanikiwa huku akimshukuru Rais Samia kwa kuipa nguvu.
“Tumekuwa wadau wakubwa sana wa Wizara ya Katiba na Sheria, sababu suala zima la upatikanaji haki na msaada wa kisheria ndiyo suala ambalo tunaishi kwa ajili hiyo na tunafurahi sana kwamba tumefanikiwa kuzindua kampeni hii ya msaada wa kisheria,” amesema Ng’wanakilala.