Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Dunia nchini Nathan Belete akizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa ripoti ya uchumi yenye jina la Maji safi na mustakabali mzuri wa mazingira ambao umefanyika jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga akizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa ripoti ya uchumi yenye jina la Maji safi na mustakabali mzuri wa mazingira ambao umefanyika jijiji Dar es salaam.
Uzinduzi wa ripoti ya Toleo la 18 la Taarifa ya Uchumi wa Tanzania, yenye jina la Maji Safi, Mustakabali MzuriThe Transformative Impact of Investing in WASH, ambayo inajadili fursa kubwa ambazo nchi inapata kupata kwa kuwekeza zaidi katika upatikanaji wa Maji, Usafi wa Mazingira na Usafi kwa wananchi wote.
……………………..
NA MUSSA KHALID
Benki ya Dunia inatarajiwa kuipa Tanzania mkopo wa masharti nafuu wa Dola za Kimarekani Mill 300 sawa na Shiling Bill 700 kwa lengo la kuboresha huduma a maji vijijini na usafi wa mazingira,Afya na elimu.
Hayo yameelezwa jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga wakati akizungumza na wanahabari katika mkutano wa uzinduzi wa ripoti ya uchumi yenye jina la Maji safi na mustakabali mzuri wa mazingira.
Mhandisi Sanga amesema malengo yao mpaka kufia mwaka 2025 huduma ya maji maeneo ya mijini ifike asilimia 95 na maeneo ya vijijini imefika asilimia 85 ambapo mwezi wa tatu watazindua ripoti ya hali ya huduma ya maji.
‘Hali ya Huduma ya maji tutaizindua mwezi wa tatu katika wiki ya maji kuanzia tar 16-22mwezi wa tatu kila mwaka ambapo tutaweza kupata matokeo mazuzi hasa maeneo mengi ya vijijini kwani wananchi wengi sasa wanapata maji’amesema Mhandisi Sanga
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Dunia nchini Nathan Belete amesema ili Tanzani akuhakikisha upatianaji wa maji kwa wote uwekezaji mkubwa unahitajika ili kuepuka matokeo mabaya ya huduma duni.
‘”Kufikia malengo ya WASH kunaweza kusaidia ajenda ya ajira huku kukipunguza athari mbaya katika tija ya wafanyakazi na kuendeleza malengo ya Tanzania ya ukuaji jumuishi na kupunguza umaskini.”amesema Belete
Kwa upande wake Dkt Ibrahim Kabole kutoka Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar na Msimamizi wa Taasisi ya Ufuatiliaji na usimamizi wa miradi ya serikali,amesema ripoti hiyo imewasaidia kupata taarifa na mafanikio ya maendeleo ya sekta ya maji ikiwa ni pamoja na vipaumbele vyake.
Hata hivyo wananchi wametakiwa kuendelea kutoa ulinzi katika miundombinu ikiwa ni pamoja na kuepukana na uharibifu wa mazingira ili kuondokana na changamoto ya ukosefu wa maji katiba maeneo mbalimbali.