Dongobesh-Mbulu.
Mkuu wa wilaya ya Mbulu Komredi Kheri James, ametembelea na kuona Mradi Mkubwa wa Upimaji wa Ardhi katika Halimashauri ya Mbulu Vijijini.
Komred Kheri James amempongeza Mkurugenzi na Baraza la Madiwani kwa Mpango huo Maalum na Muhimu kwa Maendeleo ya Mbulu.
Komred Kheri James amesisitiza kuwa ajenda ya Kupima, Kupanga na Kumilikisha Aridhi lazima iwe ni Ajenda ya Kipaumbele, ili kutengeneza Muonekano wa Mji, Kudhibiti Ujenzi Holela, Kupunguza Migogoro na Kuongeza thamani ya Aridhi kwa wamiliki.
Pamoja na Msisitizo huo Komred Kheri James ameelekeza Elimu zaidi na Ushirikishwaji wa Wananchi ufanyike ili kurahisisha Zoezi hilo Muhimu.
#Kwapamoja,tunaijenga Mbulu yetu.