Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye(Mb), ameeleza kusikitishwa kwake na tamko lililotolewa na Jukwaa la Wahariri wa HabariTanzania(TEF) hapo jana tarehe 08 Februari, 2023 likishutumu kuwa kuna ukwamishaji wa makusudi wamchakato wa marekebisho ya Sheria yaHuduma za Habari namba 12 ya mwaka 2016.
Ameeleza masikitiko hayo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari
katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Jijini Dodoma wakati akitoa
taarifa ya kusomwa kwa mara ya kwanza kwa muswada ya marekebisho ya Sheria ya Huduma za Habari namba 12 ya mwaka 2016 utakaowasilishwa katika kikao cha Bunge cha kesho tarehe 10 Februari, 2023.
Waziri Nape amesema mchakato wa marekebisho ya Sheria hiyo ulitokana na
utashi wa kisiasa wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan mara alipoingia madarakani tarehe 17 Machi, 2021 na sio shinikizo la mtu ama kikundi chochote na kwamba tangu alipotoa maelekezo ya kufanyika kwa marekebisho hayo Serikali imeshirikiana bega kwa bega na wadau
wa habari katika kufanya mapitio na hatimaye kukubaliana maeneo
yatakayofanyiwa mabadiliko.
Ameongeza kuwa katika mchakato huo, wadau wa habari wamepata fursa ya
kuwasilisha maeneo ambayo wanataka yarekebishwe, wamekutana na viongozi
wa Wizara, wamefanya majadiliano yap amoja na Serikali na ikiwemo Mhe.
Waziri kuongoza kikao cha pamoja kati ya Wizara na wadau wa habari
kilichofanyika tarehe 21 Novemba 2022ambapo waliweka makubaliano ya
pamoja ya upande wa Serikali na upande wa wadau juu ya mapendekezo ya maeneo yatakayofanyiwa marekebisho.
Waziri Nape amesema inashangaza kuona TEF inatoa tamko linaloonesha
hawakubaliani na vifungu vya muswada wa marekebisho ya Sheria unaotarajiwa
kuwasilishwa Bungeni ambao bado haujasomwa pamoja na kuwashambulia
baadhi ya Maafisa wa Serikali kwamba wanakwamisha marekebisho ya sheria hiyo.
Amesisitiza kuwa Sheria hii inawahusu wadau wote wa habari na sio kundif ulani, na hivyo amewasihi wadau wote kuaminiana, kuvumiliana na kuachav itendo vya kuzua taharuki na uchochezi ambao ni kinyume nadhamira yaS erikalikatika mchakato huu.
Aidha, amewataka kuendelea kuiunga mkonoS erikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassank atika dhamira yake ya kuboresha sekta ya habari ambapo kwa sasa kamatialiyoiunda ya kutathmini uchumi wa vyombo vya habari na kutoa mapendekezoi naendelea na kazi vizuri.
Imeandaliwa 09 Februari, 2023