Wakati Rais Dkt Samia Suluhu Hassan akitimiza takribani miaka miwili madarakani, Waandaaji wa Tamasha la Pasaka mwaka huu wameeleza kuwa licha ya Tamasha hilo Kuwa Kwenye mrengo wa Kusifu na Kuabudu, Msimu huu litajikita pia kuelezea yale mazuri yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt Samia kwa Watanzania.
Hayo yamebainisha na Alex Msama leo Februari 08, 2023 Jijini Dar es Salaam wakati akielezea kuhusiana na Tamasha hilo ambalo mara ya Mwisho lilifanyika mwaka 2015.
“Nataka niwaambie mheshimiwa Rais tokea aingie madarakani huu ni mwaka wa Pili sasa, ambapo kupitia tamasha hili kuna mambo mengi tutawaeleza Watanzania ambapo Dkt Samia ameyafanya kwa Ajili ya maendeleo ya Watanzania, pia tutamshukuru mungu kwa Ajili ya Rais wetu ampe nguvu ya kuendelea kuwatumikia Watanzania ili kuwaletea maendeleo” amesema Msama.
Akielezea kuhusiana na Tamasha la Pasaka ambalo ni Mahususi pia kwa ajili ya Kumsifu na kumuabudu mungu, Msama amesema litahudhuriwa na Waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili kutoka ndani na nje ya Tanzania ambapo limepangwa kufanyika hapa Jijini Dar es Salaam April 09 mwaka huu.