……………………….
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, SACP RAMADHANI NG’ANZI amewataka madereva wote nchini kutii sheria, taratibu, na kanuni zote za Usalama Barabarani ili kuepusha ajali zinazopelekea vifo na majeruhi nchini.
Kamanda Ng’anzi amesema hayo wakati alipotembelea eneo la tukio ilikotokea ajali maeneo ya Magila Gereza mkoani tanga.
Ajali hiyo ilihusisha magari T673 CUC Mitsubishi Fuso na T863 DXN Toyota Coaster na kusababisha Vifo 17 na majeruhi 12 huku chanzo kikielezwa kimetokana cha ajali gari aina ya Mitsubishi Fuso kulipita gari la mbele bila kuchukua tahadhari.