Katibu Msaiduzi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kanda ya Kati Dodoma Bibi Jasmini Awadhi akitoa neno katika uapisho wa Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mh Gelard Lomward Mongela kulia kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Dr. Fatma Mganga. uapisho huo umefanyika Katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma tarehe 30 januari 2023.
……………………………………….
Katibu Msaidizi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kanda ya kati Dodoma Bibi Jasmini Awadhi amewataka wakuu wapya wa wilaya walioteuliwa kuheshimu na kuviishi viapo vyao walivyoviapa kwa uadilifu na uaminifu mkubwa ktk utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Bibi Awadhi alitoa kauli hiyo alipokuwa akitoa kiapo cha Ahadi ya Uadilifu kwa Mkuu wa wilaya ya Chemba Mh Gelard Lomward Mongela katika hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Dodoma tarehe 30 January 2023.
Alisema”hakikisheni mnajitoa kutumikia viapo mlivyotoa mbele yetu na kuviweka katika kumbu kumbu zenu za kila siku ili viwasidie kuyakunbuka yale yote yaliyoelezwa katika viapo hivyo mnapotekeleza majukumu yenu ya kila siku”.
Katika hatua nyingine Bibi Awadhi alimpongeza Mkuu wa wilaua ya Chemba kwa kuteuliwa kwake na alisema kuwa Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekupa heshima ya kubwa ya kuiongoza wilaya ya Chemba.
Katibu huyo Msaidizi aliwapongeza wakuu wengine wapya wa wilaya za Bahi Mhe Godwini Gondwe na Mpwapwa Mh Sophia Kizigo waliohamishiwa mkoani Dodoma katika mabadiriko ya vituo vya wakuu wa wilaya yaliyofanyika hivi karibuni.
Hafla ya kumuapisha Mkuu wa wilaya ya Chemba na kuwakaribisha wakuu wa wilaya wapya ilifunguliwa na mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyemule ambayo pia ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa mkoa wa Dodoma, Viongozi wa dini, Viongozi wa vyama vya siasa, kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa pamoja na Menejimenti ya ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Dodoma