Mfano wa hundi ya shs 100 milioni iliyotolewa na Nabii mkuu katika soko la Samunge lililopo jijini Arusha.
Mtume ,Balozi wa Nabii mkuu Mh Dkt GeorDavie wa kanisa la Ngurumo ya upako Sekela  Ntondolo  akizungumza kwa niaba ya Nabii mkuu wakati wa kukabithi hundi hiyo katika soko la Samunge jijini Arusha.
………………………………………….
Julieth Lazier,Arusha .
Nabii mkuu Dkt GeorDavie  wa kanisa la Ngurumo ya upako leo amekabithi rasmi hundi ya shs 100 milioni kwa soko la Samunge fedha alizoahidi hivi karibuni   kwa ajili ya ukarabati na kuwasaidia wajasiriliamali wenye mitaji  midogo katika soko la Samunge lililopo kata ya  mjini kati mkoani Arusha.
Akikabithi rasmi hundi hiyo leo kwa niaba ya Nabii huyo  katika soko la Samunge ,Mtume Balozi wa Nabii  mkuu Mh.Dkt GeorDavie ,Sekela Rowland Ntondolo  amesema kuwa, Nabii GeorDavie ni msikivu na ni mtu wa watu  hivyo ametekeleza  kile alichoahidi kwa vitendo ikiwa  ni sehemu mojawapo ya kumuunga  mkono  Rais  Samia  katika kuchangia  shughuli mbalimbali za maendeleo. 
Aidha katika ahadi yake,Nabii alisema  kuwa,kiasi cha shs milioni 80 watagawiwa mtaji  wajasiriamali wenye mitaji midogo  na huku shs milioni 20 ikitumika kwa ajili ya kukaratabati  soko  hilo.
Balozi  Ntondolo amesema kuwa,watu wengi huvunja biashara zao kwa maneno yao wenyewe badala yake amewataka subiri maneno ya ushindi  katika biashara zao ili ziweze kubarikiwa na kuendelea kukua zaidi. 
“Mnatakiwa mzungumze maneno  mazuri tena kwa ujasiri mkubwa kuhusu biashara  zenu na kupitia fedha hizi mkafanye biashara  kwa bidii  huku mkimwomba Mungu mfaidi matunda ya fedha hizo  mlizopewa  na Nabii  “amesema Mtume Balozi Ntondolo.
Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa soko hilo Njola Miraji, amemshukuru nabii mkuu kwa kutimiza ahadi yake akidai kuwa wapo mabilionea waliotokana na madini ya Tanzanite lakini wameshindwa kusaidia  jamii yenye uhitaji .
Amesema katika fedha hizo wameorodhesha majina ya  wafanyabiashara 1261watakaonufaika na fedha hizo na tayari majina hayo ameyakabidhi kwa nabii mkuu kama alivyoelekeza wakati akiajidi fedha hizo . 
Naye mkuu wa soko hilo,Restituta Nyoni amewataka wafanyabiashara watakaonufaika na fedha hizo kuzielekeza kwenye biashara husika na kuepuka kuzipeleka mambo yasiofaa ikiwemo kwenye vikoba.
“Endapo utapokea hizo fedha nenda kafanye biashara usiende kunywea pombe au kuingiza kwenye vikoba”amesema Nyoni.