Naibu Waziri wa Kilimo Antony Mavunde akizungumza leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa usambazaji wa mbolea katika mikoa mbalimbali nchini kupitia Kampuni yaTFC .
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mbolea nchini -TFC Samuel Mshote akizungumza leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa usambazaji wa mbolea katika mikoa mbalimbali nchini kupitia Kampuni yaTFC .
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea nchini –TFRA Dkt Stephen Ngailo akizungumza leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa usambazaji wa mbolea katika mikoa mbalimbali nchini kupitia Kampuni yaTFC .
Mwenyekiti wa Bodi wa Kampuni ya Mbolea nchini -TFC Prof Florance Turuka Bengesi akizungumza leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa usambazaji wa mbolea katika mikoa mbalimbali nchini kupitia Kampuni yaTFC
Mkurugenzi Mkuu Bodi ya sukari Prof Kenneth Bengesi akizungumza leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa usambazaji wa mbolea katika mikoa mbalimbali nchini kupitia Kampuni yaTFC
Wajumbe wa Bodi ya Kampuni ya Mbolea nchini -TFC na Menejimenti wakati wa uzinduzi wa usambazaji wa mbolea katika mikoa mbalimbali nchini kupitia Kampuni ya TFC .
Naibu Waziri wa Kilimo Antony Mavunde akikata Utepe kuashiria uzinduzi wa usambazaji wa mbolea katika mikoa mbalimbali nchini kupitia taasisi yaTFC ambao umefanyika leo jijini Dar es salaam.(PICHA NA MUSSA KHALID)
……………………
NA MUSSA KHALID
Naibu Waziri wa Kilimo Antony Mavunde ameitaka Bodi na Menejimenti ya Kampuni ya Mbolea nchini TFC kuhakikisha wanaendesha kampuni hiyo kwa weledi na uadilifu ili kuweza kuyafikia malengo na matarajio.
Pia amesema serikali imeongeza fedha katika ufafiti wa Kilimo kutoka shilingi bilioni 11.6 Hadi shilingi bilioni 40 lengo nikumuwezesha mkulima kufanya kilimo Cha uhakika na chenye tija.
Naibu Waziri Mavunde amesema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akizindua usambaji wa Mbolea nchini katika hafla iliyofanyika kwenye eneo la Kampuni ya Mbolea Tanzania –TFC.
Aidha Naibu Waziri amewataka kupitia kazi hiyo ya usambazaji wa Mbolea kuhakikisha wanafika maeneo mbalimbali kwani ni bidhaa muhimu katika maisha ya Watu na usalama wa chakula.
‘Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa wakulima hawapati changamoto ya pembejeo na maeneo yote yasiyofikika yatafikiwa na wakulima watapata mbolea kwa haraka’amesema Naibu Waziri Mavunde
Kuhusu Kilimo cha Umwagiliaji Naibu Waziri Mavunde amesema Rais Dk Samia anataka kuiona Tanzania yote inamwagiliwa ili kuendelea kuikuza sekta ya kilimo ambapo kwa sasa wanafanya upembuzi wa kina wa kuyapitia mabonde 23 nchini.
Akieleza taarifa za utekelezaji wa majukumu ya TFC,Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo Samweli Ahadi Mshote amesema katika uzinduzi huo yameruhusiwa Malori yenye uwezo wa kusafirisha tani 210 za Mbolea na kila Lori Moja Lina mifuko 600 ambapo yameruhusiwa kwenda Mkoa wa Sumbawanga.
‘Licha ya Magari haya saba ambayo yanaondoka pia kuna magari mengine 15 ambayo yanachukua tani 450 ambapo kila moja linachukua mifuko 600 hivyo nawaomba wakulima watulie kwa kipindi hiki kwani watakwenda kunufaika na Mbolea hizi’amesema Mshote
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea nchini –TFRA Dkt Stephen Ngailo amesema watahakikisha wanashirikiana na TFC lakini pia wataendelea kutekeleza jukumu lao la kudhibiti Mbolea.
‘Niwaombe wafanyakazi wote wa Kampuni ya Mbolea Tanzania tujitahidi kwenda na Sheria ya Mbolea ikiwemo uhifadhi wa mbolea katika maeneo ambayo yanakubalika Kishera’amesema Dkt Ngailo
Hata hivyo Naibu Waziri Mavunde amesema ili kuongeza tija kwenye Kilimo serikali inakusudia kutumia zaidi ya shilingi bilioni 361 ili kuwezesha Kilimo Cha umwagiliaji Kwa kujenga mabwawa 14 kwenye mabonde 23 ikiwemo bonde la ziwa Victoria,Mto Ngono,Malagalalasi ,Ruvu na Wami ambayo yakikamilika yatakuwa nanuwezo wa kuhifadhi maji Lita bilioni 361 hivyo kuwezesha Kilimo Cha umwagiliaji