Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba Tanzania NHC Nehemia Mchechu akipongezana na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya KingJada Hotel and Apartments Bw. Praveen Toshniwal mara baada ya kusainiana mkataba wa upangaji wa hoteli katika eneo la Morocco Square jijini Dar es Salaam leo Januari 27,2023.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba Tanzania NHC Nehemia Mchechu akizungumza kabla ya kutiliana saini mkataba wa upangaji wa hoteli katika mradi wa Morocco Square jijini Dar es Salaam.
Picha zikionesha Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba Tanzania NHC Nehemia Mchechu kulia na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya KingJada Hotel and Apartments Bw. Praveen Toshniwal wakitia saini mkataba wa upangaji wa hoteli katika eneo la Morocco Square jijini Dar es Salaam leo Januari 27,2023.
Mkuu wa Mawasiliano Kampuni ya KingJada Hotel and Apartments Bw. Risasi Mwaulanga akizungumza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba Tanzania NHC Nehemia Mchechu kulia na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya KingJada Hotel and Apartments Bw. Praveen Toshniwal wakionesha nyaraka baada ya kusaini mkataba wa upangaji wa hoteli katika eneo la Morocco Square jijini Dar es Salaam leo Januari 27,2023.
Picha ya Pamja
Shihirika la nyumba Tanzania (NIC) limeingia mkataba na kampuni ya KingJada Hotel and Apartment katika eneo la Morocco Square jijini Dar es salaam kwa ajili ya huduma za hotel ya kisasa ambayo itakuwa inahudumia watu wengi kuliko hotel zote katika jijini hilo
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba Tanzania NHC Nehemia Mchechu amesema kuwa wamesaini mkataba wa uwekezaji wa HOTELI ya KingJada Hotel and Apartments Ltd Katika eneo la Morocco Square jijini Dar es salaam leo Ijumaa 27,2023 kwa mkataba wenye manufaa ya wateja wengi watakaoishi na kupata huduma katika eneo hilo muhimu.
Utiaji saini wa mkataba huu wa upangaji wa hotel ya Mradi wa Morocco Square kati ya NHC na KingJada Hotels & Apartments Ltd ni ishara ya uthubutu na imani ya sekta binafsi kwa Shirika na nchi kwa ujumla. KingJada Hotel & Apartments ni mmojawapo kati ya wawekezaji kadhaa ambao waliomba nafasi ya kuendesha hotel hii na ambaye amekidhi vigezo tulivoweka, ambavyo ni kupanga na hatimaye kununua hoteli. Mwekezaji huyu amepatikana miongoni wa wawekezaji wengi waliowasilisha mapendekezo yao ya biashara.
Nataka nimhakikishie mwekezaji huyu kuwa tutampa ushirikiano wa kutosha ili aweze kutimiza malengo yake na yetu tuliyojiwekea kwani sisi kama Shirika tunamkabidhi jengo la kisasa likiwa na huduma zote muhimu ukiwamo umeme wa uhakika, miundombinu ya zimamoto, mfumo wa vipoza joto, miundombinu ya mtandao wa mawasiliano, lifti, ulinzi wa saa 24 wa kamera za CCTV na kisima kirefu cha maji chenye mfumo wa kusukuma maji ya kutosha.
“Kwangu ni furaha kubwa siku ya leo kwa sababu inatufanya tuanze kufunga zile hatua muhimu za uwekezaji wetu ili watu waanze kutumia hizi huduma, Ingekuwa ni Kichaa ningesema NHC tumepata wazimu wa kujenga na kujenga miradi zaidi, Lakini Wazimu mzuri na wa maendeleo hii inatokana na kwamba tunayo miradi mingi ambayo tutaendeleza kuijenga karibu nchi nzima ili kuleta maendeleo katika uwekezaji wa sekta ya nyumba nchini,” Amesema Nehemia Mchechu
Mchechu ameongeza kuwa anatamani hoteli hiyo ifunguliwe wakati wa sikukuu za pasaka au Idd kwa sababu itakuwa na uwezo wa kupokea wateja wengi kuliko hotel zote jijini Dar es salaam ukizingatia kwamba eneo la Morocco Square litaweza kutembelewa na watu elfu 10.000 kwa siku moja jambo ambalo linaiweka hoteli ya KingJada kuwa katika uwezo mzuri wa kufanya biashara mara itakapoanza kazi
Mchechu ametanabaisha kuwa mojawapo ya sehemu muhimu ya mradi huo ni jengo hili linalotoa huduma za hoteli. Sehemu hii ni muhimu sana kwa sababu ndiyo inayokamilisha dhana nzima ya mradi huu ya kuishi, kufanya kazi, kununua bidhaa na kupata mapumziko mahala pamoja (live, work, shop and enjoy at the same location).
Amesema kusainiwa kwa mkataba wa upangaji na uendeshaji wa hoteli hii leo ni ishara ya kuwa katika hatua za mwisho za umaliziaji wa ujenzi na hatua za mwanzo za ufunguzi wa mradi. Hatua hii inatoa ishara kubwa na muhimu sana katika sekta ya miliki kwa kukamilisha mojawapo ya miradi mikubwa sana ya ujenzi Nchini Tanzania.
Mchechu amewashukuru wadau mbalimbali wanaoshirikiana nao katika mradi huo ambao ni Hotel & Apartments, Mkandarasi wa mradi huu (Estim Construction), wanunuzi wa nyumba na ofisi za mradi huu, wapangaji wa maeneo ya biashara ya mradi huu, wabia wa taasisi za fedha, na timu ya NHC kwa jitihada zenu zote na kazi ya kitaalamu kuwezesha hafla hii ya utiaji saini ikafanikiwa.