Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter
Kisenge akimkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Fatma Mrisho
kitabu chenye maelezo ya Taasisi hiyo wakati mkurugenzi huyo alipomtembelea
ofisini kwake leo kwa ajili ya kuona ni namna gani JKCI itashirikiana na Hospitali ya
Rufaa ya Mnazi Mmoja Zanzibar katika kutoa huduma za kibingwa za matibabu ya
moyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Fatma Mrisho akisalimiana
na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter
Kisenge alipomtembelea ofisini kwake leo kwa ajili ya kuona ni namna gani
watashirikiana na Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja Zanzibar katika kutoa
huduma za kibingwa za matibabu ya moyo kwa wananchi.
Naibu Waziri Afya Zanzibar Mhe. Dkt. Hassan Khamis Hafidh akizungumza
jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt.
Peter Kisenge alipotembelea ofisi ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo kwa ajili ya
kuona ni namna gani JKCI itashirikiana na Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja
Zanzibar katika kutoa huduma za kibingwa za matibabu ya moyo kwa wananchi.
Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Fatma Mrisho.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter
Kisenge akimkabidhi Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Dkt. Hassan Khamis
Hafidh kitabu chenye maelezo ya Taasisi hiyo wakati mkurugenzi huyo
alipomtembelea Katibu Mkuu wa wizara hiyo kwa ajili ya kuona ni namna gani
JKCI itashirikiana na Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja Zanzibar katika kutoa
huduma za kibingwa za matibabu ya moyo kwa wananchi. Kushoto ni Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Fatma Mrisho na kulia ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa Mnazi Mmoja Zanzibar Dkt. Muhiddin Abdi
Mahmoud.
””””””””””””””””””””””””’
Na Mwandishi Maalum – Zanzibar
26/01/2023 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Fatma Mrisho amesema moja ya faida za muungano ni kupatikana kwa huduma za kibingwa za matibabu ya moyo zinazotolewa na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) katika kambi maalum ya matibabu ya siku tano inayofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja Zanzibar.
Dkt. Mrisho ameyasema hayo leo wakati akiongea na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt. Peter Kisenge aliyemtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kuona ni namna gani watashirikiana na Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja Zanzibar katika kutoa huduma za kibingwa za matibabu ya moyo kwa wananchi.
Katibu Mkuu huyo alisema watu wengi wamekuwa wakiangalia kero za muungano na kusahau kuangalia faida zinazopatikana katika muungano ambazo zipo nyingi moja wapo ikiwa ni kupata huduma za matibabu.
“Katika sekta ya afya kupitia muungano wa Tanzanyika na Zanzibar wananchi wanapata matibabu pia wataalamu wanabadilishana ujuzi wa kazi kama inavyofanyika sasa ambapo wataalamu wa JKCI wako Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kutoa huduma za vipimo na matibabu kwa wananchi”,.
“Ninawashukuru sana kwa kuja kwenu Zanzibar kutoa huduma za matibabu kwa wananchi, kuwepo kwa ushirikiano huu kumesaidia pia wataalamu wetu kupata ujuzi kutoka kwa wenzao wa JKCI”, alisema Dkt. Mrisho.
Kuhusu suala la wananchi kufanya mazoezi ili kujikinga na magonjwa yasiyo ya kuambukiza yakiwemo magonjwa ya moyo Dkt. Mrisho alisema wananchi wa Zanzibar wanajitahidi sana kufanya mazoezi kwani kuna vikundi vingi vya mazoezi vikiwemo vya wanawake, hivi sasa watu wanatambua kufanya mazoezi ni kuzuri siyo tu kwa vijana bali hata kwa wazee.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Amour Suleiman Mohammed alisema wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete wanafanya kazi kubwa ya kutibu wagonjwa wa moyo na wamepunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya wagonjwa waliokuwa wanaenda nje ya nchi kutibiwa.
“JKCI imepunguza idadi ya wagonjwa waliokuwa wanapelekwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kutibiwa maradhi ya moyo nchini India, Serikali imepunguza gharama na hivi sasa wagonjwa wote wa moyo tunawapeleka kutibiwa JKCI na siyo India kama ilivyokuwa zamani, na wagonjwa wanafurahi kwa huduma wanayoipata”,.
“Miaka ya hivi karibuni tumekuwa na kambi za pamoja za matibabu ya kibingwa ya magonjwa mbalimbali zinazofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja Zanzibar, kuwepo kwa kambi hizi kumewapunguzia wananchi gharama za safari ya kuzifuata huduma hizo Dar es Salaam”, alisema Dkt. Mohammed.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge alisema Taasisi hiyo imekuwa ikitoa huduma ya kibingwa ya matibabu ya moyo ya kuwafuata wananchi mahali walipo ambapo kwa mwaka huu wa 2023 wameanza kutoa huduma hiyo katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Zanzibar na mwaka ujao wa fedha watakwenda Kisiwani Pemba.
Dkt. Kisenge alisema lengo la kutoa huduma hiyo ni kuhakikisha wananchi hasa wa maeneo ya pembezoni mwa Tanzania wanapata huduma ya kibingwa ya matibabu ya moyo kwa wakati kwani changamoto kubwa wanayokutana nayo ni wagonjwa wengi wanaofika kutibiwa katika Taasisi hiyo mioyo yao inakuwa imechoka.
“JKCI imekuwa ikiwapokea wagonjwa wengi kutoka Zanzibar nasi tukaona tuwafuate wananchi huku waliko ili wapate huduma hii, pia tutashirikiana na Hospitali ya Rufaa Mnazi Mmoja Zanzibar kitengo cha moyo kwa kubadilishana ujuzi wa kazi na wenzetu wa hapa ili nao wawe na utaalamu kama tuliokuwa nao sisi”, alisema Dkt. Kisenge.
Wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kkwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar wanafanya kambi maalum ya matibabu ya moyo ya siku tano kwa watoto na watu wazima katika Hospitali hiyo ambapo kwa muda wa siku nne wameweza kuona watu 555 kati ya hao watu wazima 485 na watoto 70, waliokutwa na matatizo yaliyohitaji matibabu ya kibingwa na kupewa rufaa ya kwenda kutibiwa JKCI 55