Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Mufindi George Kavenuke akionyesha kadi ya CHADEMA aliyokabidhiwa na ayekuwa mwenyekiti wa CHADEMA kata ya Mapanda Isaya Kitinusa
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Mufindi George Kavenuke akipokea kadi na videndea kazi vya chama hicho kata ya Mapanda baada ya wanachama wa kuhamia CCM
Katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Mufindi Dikson lutevele akiwa na Isaya Kitinusa aliyehamia CCM akitokea CHADEMA kata ya Mapanda
Na Fredy Mgunda, Iringa.
CHAMA cha mapinduzi CCM wilaya ya Mufindi kimempokea mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) na wenzake zaidi ya 20 katika kata ya Mapanda.
Akizungumza wakati wa ziara kuimarisha chama, mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mufindi George Kavenuke alisema kuwa wamempokea aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA kata ya Mapanda na wenzake baada ya kuridhika kutokana na utendaji wa kazi wa viongozi wa chama cha mapinduzi.
Kavenuke alisema kuwa diwani wa kata ya Mapanda Obadia Kalenga amekuwa anafanya kazi nzuri ambayo imekuwa ikiwavutia watu wengi wakiwemo wapinzani ambao sasa wameamua kuungana na chama hicho.
Alisema kuwa ukiwa na viongozi wa kata kama diwani Obadia Kalenga ambao wanatekeleza Ilani ya chama cha mapinduzi CCM inavyotakiwa inasaidia kukijenga chama kuanzia ngazi ya shina hadi Taifa.
Kavenuke alimkaribisha Isaya Kitinusa katika chama cha mapinduzi kwa ajili ya kufanya nao kazi kwa kuwa chama cha mapinduzi ndio chama cha mfano katika Bara la Africa na duniani kwa namna ambavyo kinaendesha siasa zake.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Mapanda Obadia Kalenga alisema kuwa amekuwa anafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na wananchi wote wa kata ya hiyo ndio maana wapinzani wamekosa sehemu ya kukosoa ndio maana wamerudi katika chama cha mapinduzi.
Kalenga alisema kuwa sio mara kwanza wapinzani kutoka chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kujiunga na CCM katika kata hiyo hilo limekuwa linajitokeza kila wakati toka amechaguliwa kuwa Diwani wa kata ya Mapanda.
Alisema kuwa ataendelea kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi na kutekeleza Ilani ya chama cha mapinduzi CCM kama ambavyo inavyotaka ili kuwaletea maendeleo wananchi wa kata ya Mapanda.
Naye katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Mufindi Dikson lutevele alisema kuwa ataendelea kufanya ziara za kutoa elimu ya namna ambavyo CCM inafanya kazi zake ili kuwavutia wapinzani wajiungu na chama hicho.
Lutevele alisema kuwa chama cha mapinduzi CCM ndio chama kikubwa na chenye misingi imara ya kuwaletea maendeleo wananchi kuliko chama chochote kile hivyo wananchi wanatakiwa kuendelea kukiamini chama hicho kuendelea kushika madaraka.
Isaya kitinusa alisema kuwa ameamua kurudi CCM Mara baada ya kuona chama hicho kinafanya shughuli mbalimbali za kimaendeleo kwa wananchi na kukuza uchumi tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Kitinusa alisema kuwa yupo tayari kukitumikia chama hicho kwa nguvu zote na kuondoa kabisa upinzani katika kata ya Mapanda ili kumsaidia diwani wa kata hiyo kufanya kazi za kimaendeleo bila kusumbuliwa na wapinzani.