Mkurugenzi wa Plan International Tanzania Bi. Mona Girgis (kushoto) akikabidhi sehemu ya vitabu 10,120 kwa mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mhe. Sebastian Waryuba (kulia) jana katika hafla iliyofanyika shule ya msingi Milundikwa wilaya ya Nkasi.
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mhe. Sebastian Waryuba akizungumza na jumuiya ya shule ya msingi Milundikwa wilaya ya Nkasi jana wakati alipopokea msaada wa vifaa vya elimu kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Rukwa vilivyotolewa na shirika la Plan International Tanzania.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Peter Lijualikali (kulia) akipokea sehemu ya vitabu 10,120 toka kwa mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Sebastian Waryuba vilivyotolewa na shirika la Plan International kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi (29) za Nkasi.
Mkurugenzi wa Plan International Tanzania Bi. Mona Girgis (kushoto) akikabidhi sehemu ya vitabu 10,120 kwa mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mhe. Sebastian Waryuba (kulia) jana katika hafla iliyofanyika shule ya msingi Milundikwa wilaya ya Nkasi.
Moja ya choo shirikishi kati ya 17 vilivyojengwa na shirika la Plan International Tanzania kwa ajili ya wanafunzi katika shule za msingi 7 na sekondari 9 kwenye halmashauri za Nkasi, Kalambo na Sumbawanga vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 716 kama kinavyoonekana katika shule ya msingi Milundikwa wilaya ya Nkasi jana.
Na. OMM Rukwa
Shirika la Plan International Tanzania limekabidhi msaada wa vitabu, vyoo
shirikishi na miundombinu ya maji kwa shule za sekondari na msingi kwenye
Halmashauri za Wilaya Nkasi, Kalambo na Sumbawanga vyenye thamani ya
shilingi Milioni 786 .
Halfa ya makabidhiano ya msaada huo imefanyika katika shule ya msingi
Milundikwa wilaya ya Nkasi jana (Januari 19,2023) ambapo Mkuu wa Wilaya
ya Sumbawanga Sebastian Waryuba alipokea msaada huo kwa niaba ya
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga.
Waryuba akizungumza kwenye hafla hiyo alitoa pongezi kwa shirika hilo kwa
kuchangia vyoo shirikishi 17 na miundombinu ya maji katika shule za msingi 7
na sekondari 9 katika Wilaya za Nkasi, Sumbawanga Vijijini na Kalambo
vyenye jumla ya thamani ya shilingi za kitanzania 716, 607, 527.
Plan International imetoa pia vitabu vya kiada 10, 128 kwa shule za msingi
29 za wilaya ya Nkasi vyenye thamani ya shilingi za kitanzania 70, 210, 000
vitakavyotumika kufundishia na kujifunzia wanafunzi na walimu.
“Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa unaofanywa na Shirika la
Plan International kwa kushirikina na Serikali katika kujenga uwezo na
kuboresha upatikanaji wa elimu bora kwa shule za msingi na awali katika
Mkoa wa Rukwa na kuleta maendeleo ya watanzania katika sekta mbalimbali
za kijamii, alisema Waryuba.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Plan International Tanzania Mona Girgis
alisema lengo la shirika ni kuhakikisha elimu bora inatolewa kwa wanafunzi
hususan watoto wa kike ndio maana linashirikiana na serikali kuboresha
miundombinu ikiwemo vyoo bora na safi na vitabu.
Mkurugenzi huyo alisema pia shirika limefanikiwa kutoa mafunzo ya kusoma,
kuandika na kuhesabu (KKK) kwa walimu wa darasa la kwanza na la pili
wapatao 48 kutoka shule za msingi 22 zilizopo kwenye kata 5 za Nkandasi,
Mashete, Mkwamba, Kate na Mtenga wilaya ya Nkasi.
Kwa upande wake Angela Kayawe ( 14) mwanafunzi wa Darasa la Saba
shule ya msingi Milundikwa alitoa shukrani kwa shirika la Plan International
kwa msaada walioutoa utakaosaidia kuimarisha taaluma mingoni mwa
wanafunzi.