Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Tarehe 19/01/20223 imefanya kikao cha Tathimini ya
walioripoti na kuanza Elimu ya awali na Darasa la kwanza katika Shule za Msingi, na Kidato
cha kwanza katika shule za Sekondari Wilayani Nyasa.
Kikao hiki kimefanyika katika Ukumbi wa Kepten John Komba, Mjini Mbamba bay na
kuwakutanisha Viongozi wa Vijiji,Kata, Wakuu wa Idara na Kamati ya Ulinzi na Usalama
Wilayani hapa.
Mgeni Rasmi katika kikao hicho ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mh.Aziza
Mangosongo Akifungua Kikao, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Nyasa amesema Lengo la Kikao ni kuhakikisha
kuwa wanafunzi wote waliochaguliwa kwenda Sekondari, na waliotimu umri wa kuanza Elimu ya
awali na darasa la kwanza wanaanza na kuacha Visingizio.
Amewataka Viongozi wa Vijiji, Kata na Halmashauri kwa ujumla kuendesha Msako wa Nyumba
hadi nyumba na kutowaachia walimu peke yao.
Amefafanua kuwa, Viongozi hawa ndio wanaoishi na jamii na kuwafahamu wakazi wao, na
kujua kuna watoto wanaotakiwa kwenda shule.
“Ninyi Viongozi wa Vijiji na kata yaani Watendaji wa Vijiji, na Kata mnaishi na wananchi na
mnawafahamu wanafunzi wote waliofaulu kuingia kidato cha kwanza, na waliotimia Umri wa
Kuanza darasa la Awali na la kwanza Wilayani Nyasa, hivyo tunatakiwa kuhamasisha jamii
kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanakwenda shule.
Mh.Mangosongo amempongeza Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa Kuipa miradi
ujenzi wa Madarasa Wilaya ya Nyasa na kutatua kero za miundombinu ya elimu.
Awali Wakitoa Taarifa ya wanafunzi walioripoti na kuanza masomo katika Shule ya Msingi,
Mkuu wa Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi Mwl Hossein Mghewa amesema Wanafunzi
walioanza masomo ni asilimia 101 kwa darasa la Awali na Asilimia 102 kwa darasa la kwanza
hivyo amemhakikishia Mkuu wa Wilaya kuwa bado wanaendelea na uhamasishaji, lengo ni
kuhakikisha kuwa wanavuka lengo kwa asilimia nyingi.
Akiwakilisha Taarifa ya Elimu Sekondari Kaimu Mkuu Divisheni ya Elimu ya Sekondari Mwl Aus
Limia amesema asilimia 44 ya wanafunzi ndio walioanza masomo ya kidato cha kwanza hadi
kufikia tarehe 18/01/2023.
Kikao kimeazimia kufanyika kwa uhamasishaji na elimu kupitia vikao vya WDC na Vijiji na
kuanza Msako wa Nyumba hadi nyumba na kuhakikisha wanafunzi wote ndani ya wiki mbili
wawe wameripoti shuleni kwa asilimia 100.
Kwa upande wake Viongozi wa Vijiji na Kata wamemhakikishi Mkuu wa Wilaya ya Nyasa
kufanya msako na kuhakikisha wanafunzi hao wanaenda shule na zoezi hili kuwa endelevu.