Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani
Jafo akisaini kitabu cha wageni alipowasili Ubalozi mdogo wa Tanzania nchini Dubai
kabla ya kikao na watendaji wakuu wa kampuni ya BLUE CARBON leo Januari 19,
2023.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani
Jafo akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzani Dubai baada ya kikao na
watendaji wa wakuu wa kampuni ya BLUE CARBON leo Januari 19, 2023.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt.
Selemani Jafo amesema kwa sasa inaifungua Tanzania katika uwanja mpana wa
mazingira duniani kwa kupitia biashara ya kaboni.
Dkt. Jafo amesema hayo leo Januari 19, 2023 nchini Dubai wakati wa vikao
mbalimbali vya kubadilishana mawazo ktk masuala ya biashara ya kaboni
ambayo tayari Tanzania imeshaandaa kanuni na mwongozo wake.
Akiwa kwenye kikao na Balozi wa Tanzania Dubai, Dkt. Iddi Seif Bakari pamoja
na watendaji wakuu wa kampuni ya Blue Carbon ya Dubai Mhe. Dkt. Jafo
amesema ziara hiyo ni mwendelezo wa maelekezo ya Serikali ya Tanzania katika
nyanja mbalimbali za kiuchumi.
“Ziara hii ni mwendelezo uleule wa maelekezo ya Serikali ya Mhe. Dkt Samia
Suluhu Hassan kuifungua Tanzania katika nyanja mbalimbali za kiunchumi na
kwa sasa inaifungua Tanzania katika uwanja mpana ya mazingira,” amesisitiza.
Alisema Serikali ya Tanzania imeshakamilisha mwongozo na kanuni za biashara
ya kaboni inatarajiwa kuongeza pato la Taifa kwa siku chache zijazo kuiweka
Tanzania katika sura nzuri ya kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendelea na
kimazingira kwa lengo la kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
“Uzingatiaji na utekelezaji wa kanuni na mwongozo huo utasaidia kuboresha
usimamizi mzuri wa miradi ya biashara ya kaboni inayotekelezwa ndani ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sekta zote,” Amesema.
Hivyo, Dkt. Jafo amesema kuwa utekelezaji wa biashara ya kaboni utachangia
kupunguza gesijoto zinazosababisha ongezeko la joto duniani na hatimae
kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi.
Waziri huyo ameongeza kuwa pia biashara hiyo itachangia katika utunzaji
endelevu ya mazingira na kuleta maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi.