Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Eng. Godfrey Kasekenya, akitoa taarifa ya
utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya Sekta ya Ujenzi kwa wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mheshimiwa Selemani
Kakoso, akisisitiza jambo kwa viongozi na watendaji wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya
Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) (hawapo pichani), mara baada ya kuwasilisha
taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayoendelea kwa mwaka wa fedha
2022/23, jijini Dodoma.
Baadhi ya Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu na Viongozi wa
Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), wakifatilia kwa makini taarifa ya
utekelezaji wa miradi ya maendeleo kutoka kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,
Eng. Godfrey Kasekenya, wakati akiwasilisha kwa Kamati hiyo, jijini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ambaye ni
Mbunge Jimbo la Same Mheshimiwa Anne Kilango, akichangia hoja wakati wa Wizara
ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) ikiwasilisha taarifa ya utekelezaji kwa Kamati
hiyo, jijini Dodoma.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ambaye ni Mbunge Jimbo la
Gairo Mheshimiwa Ahmed Shabiby, akichangia hoja wakati wa Wizara ya Ujenzi na
Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), ikiwasilisha taarifa ya utekelezaji kwa Kamati hiyo, jijini
Dodoma.
……………………………………………..
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeiagiza Wizara ya Ujenzi
na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), kuhakikisha inazisimamia Taasisi zake
kutekeleza majukumu yao katika ujenzi, ukarabati na matengenezo ya
miundombinu ya barabara, madaraja, vivuko, viwanja vya ndege, nyumba
na majengo ya Serikali.
Akizungumza jijini Dodoma, katika kikao cha kupokea na kujadili kuhusu
utekelezaji wa Bajeti ya Maendeleo ya Sekta hiyo kwa kipindi cha nusu
mwaka cha Julai hadi Desemba iliyosilishwa kwa Kamati hiyo,Mwenyakiti
wa Kamti hiyo, Mheshimiwa Selemani Kakoso, amesema kuwa pamoja na
mambo mengine amesisisitiza umuhimu wa Sekta hiyo kuongezewa fedha
ili kutekeleza na kumaliza miradi hiyo kwa wakati.
“Niipongeze Serikali kwa kuendelea kutoa fedha kwa miradi inayoendelea,
Tumeshuhudia baadhi ya miradi kukamilika na mengine kuendelea na
utekelazaji wake katika mikoa mbalimbali nchini, hivyo naiomba Serikali
iendelee kuitengea fedha za kutosha Sekta hii ili iendelee kutekeleza na
kukamilisha miradi iliyopanga”, amesema Kakoso.
Aidha, ameiagiza Wizara kuiwezesha Wakala wa Ufundi na Umeme
(TEMESA), kuweka mpango madhubuti wa kununua vipuri vya jumla
kupitia kwa Makampuni halisi ya magari badala ya kupitia kwa mawakala,
hali inayopelekea kwa Wakala kushindwa kufanya matengenezo ya
washitiri wake kwa wakati.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Eng. Godfrey Kasekenya,
ameaiahidi Kamati hiyo kuendelea kutekeleza miradi yote kwa ufanisi kwa
kuzingatia vipaumbele vilivyoweka pamoja na Ilani ya CCM ya Mwaka
2020.
Kasekenya, ameongeza kuwa Wizara (Ujenzi) kwa kushirikiana na Wizara
ya Fedha na Mipango itahakikisha kuwa fedha za Makandarasi
wanaojenga miundombinu mbalimbali inayotekelzwa na kusimamiwa na
Sekta hiyo nchini zinalipwa kwa wakati.
Naye, Mjumbe wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Gairo,
Mheshimiwa Ahmed Shabiby, ameupongeza Wakala wa Barabara
Tanzania (TANROADS) kwa kujenga na kukarabati barabara nchini
ambapo ametolea mfano wa barabara ya Morogoro – Dar eneo la Gairo
lililokarabatiwa hivi karibuni.