Naibu Makamu Mkuu wa Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA)
upande wa Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Maulid
Mwatawala wakati akifungua Mkutano Mkuu wa wa tatu wa Mwaka
wa Mradi huo uliofanyika visiwani Zanzibar.
Mkuu wa Mradi wa FoodLAND kwa upande wa Tanzania Prof. Susan
Nchimbi Msolla Kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo
akizungumzia malengo yay a Mkutano huo.
Mratibu wa Mradi wa FoodLAND kwa nchi zote washiriki Prof. Marco
Setti kutoka Chuo Kikuu cha Bologna cha nchini Italy akieleza kwa
ujumla malengo ya mradi ,utekelezaji wake mpaka sasa na Matarajio
ya mbele.
Picha ya Pamoja ya Washiriki wa mradi na mkutano huo kutoka nchi mbalimbali Duniani.
……………………………………………………
Na: Amina Hezron na Calvin Gwabara – Zanzibar.
Imeelezwa kuwa matokeo yote mazuri ya Mradi wa Chakula Kilimo na
Lishe (FOODLAND) yaliyopatikana kwenye nchi zinazotekeleza mradi huo
yatakwenda kuisaidia jamii katika kuhusanisha Kilimo, Matumzi ya mazao
ya chakula na lishe na hivyo kupunguza changamoto za chakula na lishe
Afrika.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Makamu Mkuu wa Kikuu cha Sokoine cha
Kilimo (SUA) upande wa Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Prof.
Maulid Mwatawala wakati akifungua Mkutano Mkuu wa wa tatu wa Mwaka
wa Mradi huo uliofanyika visiwani Zanzibar wa kufanya tathimini ya kazi
zilizofanyika ndani ya mradi ili kuendelea kuboresha ufanyaji kazi wa
mradi huo.
“Mradi huu unaunganisha kwanza uzalishaji wa chakula lakini pia na
matumizi ya chakula kwa sababu kumekuwa na miradi mingi ambayo
imekuwa ikiangalia uzalishaji tu pekee na miradi mengine mingi ikiangalia
matumizi ya chakula pekee kwa hiyo kunakuwa hakuna muunganiko au
uhusiano kati ya uzalishaji na matumizi ya chakula. Inawezekana chakula
kinazalishwa sana kuliko kinavyoliwa au kinacholiwa zaidi si
kinachozalishwa kwa kiwango kile ambacho kinahitajika”, alisema Prof
Mwatawala.
Prof. Mwatawala amesema amefurahishwa sana na Mchanganyiko wa
wadau wanaotekeleza mradi huo kwa kuwa unawahusisha Watafiti,
Wajasiriamali na Wabunifu maana mwisho wa utafiti matokeo hayo
yatawahusu watu hao katika makundi yao na watatakiwa kufanya kazi zao
kwa kuzingatia matokeo yatakayopatikana kwakuwa ndio njia ya kufikia
mapinduzi ya nne ya viwanda.
Akizungumzia malengo ya Mradi wa FoodLAND, Mkuu wa Mradi huo kwa
upande wa Tanzania Prof. Susan Nchimbi Msolla Kutoka Chuo Kikuu cha
Sokoine cha Kilimo amesema unalenga hasa uboreshaji wa kilimo ili watu
waweze kulima kilimo chenye tija na kinachohifadhi mazingira na
kuzingatia lishe.
“ Tunalenga kuoanisha kati ya kilimo na lishe mara nyingi tumekuwa
tukiona kwamba tunazalisha chakula kingi sana lakini wakati mwingine
sehemu hizo hizo zinazozalisha chakula kingi lishe yao ni duni kwa hiyo sisi
kwenye mradi huu tunataka tuweze kuoanisha uzalishaji wa chakula ili nchi
yetu iwe na watu wenye lishe bora”, alisema Prof Msolla.
Aidha Prof. Msolla amesema kuwa mradi huo unataka kuwa na Bioanuai ya
vyakula na mazao yanayolimwa kwa kuwa imekuwa ikionekana katika
sehemu zingine kutokana na tabia za ulaji watu wanakula vyakula vya aina
chache ingawa kuna uwepo wa vyakula vingi vinavyozalishwa huku vingine
vikiuzwa na wenyewe wanaozalisha hawavili.
“Tunataka tuweze kuongeza uwelewa zaidi kwa wakulima na walaji na ndio
maana katika mradi huu katika hatua zetu za mwanzo tuliweza kufanya
madodoso na wakulima na walaji wa vyakula mijini na vijijini ili tuweze
kujua tabia za ulaji zikoje na kwanini watu wanachagua vyakula
wanavyokula”, alisema Prof. Msolla.
Mtafiti huyo mkuu wa Mradi ameeleza kuwa matokeo ya Utafiti huo
yatasaidia katika kuboresha na kushauri watu namna ya kulima, aina ya
mazao ya kulima,kilimo cha aina gani kitumike na aina gani ya vyakula
watu wale ili kuboresha afya zao .
Akieleza kwa ujumla malengo ya mradi ,utekelezaji wake mpaka sasa na
Matarajio ya mbele Mratibu wa Mradi wa FoodLAND kwa nchi zote
washiriki Prof. Marco Setti kutoka Chuo Kikuu cha Bologna cha nchini
Italy amesema mkutano huo ni fursa kubwa kwa washiriki wote kukutana
pamoja na kubadilishana maarifa na mbinu za utekelezaji ili kufikia
malengo tarajiwa.
Amesema kumekuwa na maendeleo makubwa na mazuri ya utafiti kwenye
nchi zote wananchama kasoro Ethiopoa ambako kuna kuchelewa kwa
utekelezaji wa kazi mbalimbali kutokana na changamoto mbalimbali za
nchi hiyo lakini wana Imani kuwa nao watakamilisha na kupata matokeo.
“Tayari tumeshazalisha takribani matokeo 30 na kuyawasilisha kwa
wafadhili wetu ambao umoja wa Ulaya(European Union) ambayo
yanapatikana kwenye tovuti ya mradi na kwenye tovuti ya Umoja wa Ulaya
na kila mmoja anaweza kuyaangalia kujua kilichopatikana yapo mengine 7
yaliyozalishwa mwezi mmoja uliopita na mengine matano yanayohusu
miongozo na zana za kufundishia yanaendelea kukamilishwa” alisema Prof.
Seti.
Mradi wa FoodLAND ulianza kutekelezwa mwezi wa tisa mwaka 2020,
ukishirikisha wadau 26 kutoka nchi 13 ambapo za Afrika inawakilishwa na
Tanzania,Kenya,Uganda,Ethiopia, Tunisia, Morocco ambapo kwa mara ya
kwanza wanakutana Tanzania kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka wa mradi
huo baada ya miaka miwili yote kufanyika kwa njia ya mtandao kutokana
na changamoto za ugonjwa wa UVIKO 19.
Picha mbalimbali zinionesha washiriki wa mkutano huo wakifuatilia ufunguzi wa Mkutano.