Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Daniel G. Chongolo ameongoza Mkutano wa kwanza wa kawaida wa kamati ya uongozi katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere Mkoani Pwani leo tarehe 17 Januari, 2023.
Akitoa taarifa ya mkutano huo Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa Ndugu Sophia Mjema amesema kuwa Mkutano huu unajumuisha makatibu wakuu na wawakilishi wa vyama sita Rafiki vya ukombozi kusini mwa Afrika.
Vyama hivyo ni CCM kutoka hapa Tanzania, FRELIMO kutoka nchini Msumbiji, ZANU-PF kutoka nchi ya Zimbambwe na MPLA kutoka nchi ya Angola, SWAPO kutoka nchi ya Namibia na ANC ya Afrika kusini.
Aidha amesema kuwa Lengo la Mkutano huu ni makatibu wakuu na viongozi wengine kutembelea na kukagua miundombinu ya Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere pamoja na kupitia na Kujadili taarifa mbalimbali kuhusu uendeshaji wa chuo hiki.
Pamoja na hayo ameeleza kuwa Moja ya malengo ya kuanzishwa kwa shule hii ya uongozi ni kuandaa na kufundisha uongozi na uzalendo kwa Makada na wananchi ili kuendelea kujikomboa kiuchumi, kisiasa, kijamii na kifikra mara baada ya Ukombozi uliyofanyika wa kuondoa utawala wa kikoloni na kupata uhuru kamili.
Mukutano huu umeanza leo tarehe 17 Januari, 2023 na utamalizika tarehe 19 Januari, 2023.