Na Mwandishi Wetu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe Dkt. Selemani JAFO leo 14.01.2023 amefanya Ziara Kata ya Boga,
Katika Ziara Hiyo ameambatana na viongozi mbalimbali akiwemo Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Direct Aid Ndg. Mohamed Orab, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Ndg. Peter P. Ngussa, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kisarawe Comrade Khalfani Shabani Sika, Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Greyson Mramba pamoja na Mhe. Chakachaka ambaye ndiye Diwani wa Kata ya Boga.
Aidha Mhe. Dkt. Jafo amelipongeza na kulishukuru Shirika la Direct Aid kwa ushirikiano uliotukuka kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe,
“Direct Aid mmefanya vitu vingi kisarawe, mmetoa Solar Power, hili la kutujengea Zahanati kwetu wana Kisarawe ni Jambo Kubwa mno tutaonesha nasi ushirikiano wa kutosha katika Masuala ya Afya,Elimu,na Ushirikiano katika Ufugaji wa Mbuzi,Ngombe,Nk”
“Nakumbuka Direct Aid Kisarawe mmetufanyia Makubwa Kama wadau wa Maendeleo ya Jamii kata ya Kurui, mzenga,Boga na Maneromango. Bunafsi michango yenu kwa Wilaya yetu na Wananchi wetu tunaithamini, kuifurahia na tunawapongeza sana kwa kutusaidia sisi-Wana kisarawe Na pia Msichoke katika sekta nyengine mnazoweza kuchangia Kisarawe alimalizia Dkt. JAFO”
Kwa ujumla msaada wenu wa Maendeleo ya Jamii kwetu Kama zile Mashine na maduka ya biashara kwa Wale ndugu zetu wa Jumuia ya Walemavu Kisarawe, miradi ya ujenzi wa visima vya Maji, Bado Ni Jambo jema Sana na tunaendelea kuheshimu mno Juhudi zenu kwetu. Sisi viongozi wote wa Wilaya ya Kisarawe tutaendelea kushirikiana nanyi kwa muda wote alisisitiza mhe Dkt. Jafo
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Direct Aid Ndg. Mohamed Orab Amesema toka walipoingia Wilayani Kisarawe mwaka 2020 wameendelea kushirikiana vyema na wananchi wa Kisarawe na kwasasa wapo tayari kuanza Ujenzi wa Zahanati ya Boga na Ujenzi utaanza rasmi ndani ya Wiki moja kutoka tarehe leo
Sisi Kama ActionAid tunakuhakikishia Mhe Waziri na Watu Wako wa kisarawe Tupo Tayari Kuanza Ujenzi mda Wowote Kutoka Sasa Na Pia tunaomba Ushirikiano wa karibu na Ofisi ya Mkurugenzi kufanikisha Hili aliomba Ndugu Orab
Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kisarawe Ndg. Peter Ngussa amelishukuru Shirika la Direct Aid na kusema Kujengwa kwa Zahanati hiyo itakuwa Mwarobaini wa Changamoto kwa wananchi,
“Sasa wananchi wengi wa kijiji cha Boga, Ngongere, Mengwa na Chale watanufaika na ujenzi wa Zahanati hiyo ya Boga pamoja na kuahidi Kutoa Ushirikiano wa karibu kutoka Ofisi ya Mhandisi wa Wilaya alimalizia Ndg. Peter Ngussa”
Aidha, Diwani wa kata ya Boga Mhe. Inadi Chakachaka ameshukuru sana msaada huo wa ujenzi wa zahanati kwani utawapunguzia kina mama wa Kata hiyo umbali kwa kwenda kutibiwa ktk Kituo cha Afya Maneromango