Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Bw. Abdulmajid Nsekela akizungumza katika uzinduzi wa mfuko wa Faida Fund uliofanyika kwenye ukumbi Julius Nyetere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Januari 14, 2023.
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais , Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh. Jenista Mhagama akizungumza wakati akizindua mfuko wa Faida Fund kwenye ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Waziri wa Nchi ofisi ya Rais , Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh. Deodatus Ndejembi akimkaribiaha Waziri Jenista Mhagama ili kuzindua mfuko huo
BENKI ya CRDB imekuwa kinara nchini Tanzania Katika kutoa huduma za uwekezaji kwenye masoko ya fedha na mitaji ambapo benki imekuwa Daraja la kuwaunganisha wawekezaji wanaotafuta mitaji na wanaowekeza mitaji kwa ajili ya faida ya Taifa.
Akizungumza Katika uzinduzi wa mfuko wa pamoja wa uwekezaji FAIDA FUND uliofanyika kwenye ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela almesema kuwa benki ina idara maalum kwa ajili ya kushughulikia shughuli mbalimbali za masoko na mitaji ya ndani ya nchi na nje ya nchi.
Bw. Nsekela almesema kuwa benki imewekeza kwenye mifumo ya kisasa ya Tehama ambayo inawezesha kutoa huduma katika nchi zote duniani kwa ushirikiano wa taasisi mbalimbali za kifedha za ndani ya nchi na nje ya nchi.
Alisema kuwa kwa sasa wanawateja kutoka mataifa mbalimbali ambao wanawekeza nchini kupitia benki ya CRDB na kusimamia amana zaidi ya trillion 9.
Nsekela amesema kuwa Kuna wateja zaidi ya laki tatu ambao wamewekeza mifuko ya uwekezaji kwa pamoja kwenye benki ya CRDB,wateja zaidi ya elfu nne hati fungani za serikali na kampuni binafsi na wateja zaidi ya Laki nne wamewekeza kwe hisa kupitia kampuni mbalimbali ambazo zinafanya kazi na benki ya CRDB.
Almesema kuwa inachangia zaidi ya asilimia 70 ya wateja wote wanaoshiriki katika masoko,mitaji,dhamana nchi na soko la hisa linaitambua benki ya CRDB kuwa kinara kwenye soko la mitaji ambapo zaidi asilimia 85 benki CRDB imesaidi katika ukusanyaji wa mitaji.
Nsekela ameongeza kuwa anaipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha diplomasia ambapo wawekezaji wengi kutoka mataifa mbalimbali wamerudi kuwekeza nchi.
Amesema kuwa benki ya CRDB imejipanga kuhakikisha mfuko wa FAIDA FUND unakuwa mfuko unaowawezesha wawekezaji kuwekeza nchi kwa ushirikiano mkubwa na Watumishi Housing Investiment
Nsekela almemaliza kwa kusema kuwa anawashukuru watumishi Housing kwa kuiamini benki ya CRDB kusimamia mfuko wa FAIDA FUND jambo ambalo limekuwa kubwa na faida kwa pande zote.