Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Mhe. Omar Said Shaaban amelishukuru Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwa kupeleka Nishati Mbadala ya Mkaa unaotokana na Makaa ya Mawe Rafiki Briquettes kisiwani Zanzibar
Mhe. Waziri ameyasema hayo alipokutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt. Venance Mwasse katika viwanja vya Maisara wakati wa Tamasha la Biashara linalofanyika visiwani Zanzibar.
Ameitaka STAMICO kuainisha mawakala ambao wataendelea kupeleka mkaa huu huko Zanzibar na kujiwekeza vizuri ili biashara hii iwe endelevu kwani mkaa huu utakuwa mkombozi wa mazingira.
Waziri ameishukuru STAMICO kwa kuendelea kuwa wadhamini wa Tamasha hili la biashara kwa mara ya pili mfululizo na kuomba kuendelea kushirikiana na waandaji na kushirika katika Tamasha la mwaka 2024 ambapo Zanzibar itatimiza Miaka 60 ya Mapinduzi.
Ametumia fursa hiyo kuikaribisha STAMICO katika
Tamasha la mwaka 2024 ambalo linatarajiwa kuwa kubwa ikiwa ni sehemu ya kusheherekea kutimiza miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO amemshukuru Wizara kwa kuendelea kufanya kazi na STAMICO na kuahidi kuendelea kushirikiana na Wizara katika Tamasha la Biashara linalotajiwa kufanyika mwaka kesho.
“Nimeabiwa mnategemea kuhamia kwenye eneo lenu wenyewe la kudumu la kufanyia Tamasha la biashara na Maonesho.
Naahidi kuendeleakufanya kazi kwa pamoja kwa maendeleo yetu” aliongeza Mwasse.
Aidha Mwasse amesema STAMICO ipo tayari kushiriki katika suala nzima la utunzaji wa mazingira kwa kusaidia kupanda miti ili Zanzibar kwenye eneo leo jipya ili liwe kijani kama kampeni yao ya kutambulisha Mkaa Mbadala wa Rafiki Briquettes yenye kauli mbiu ya “Panda Mti Tumia Mkaa Mbadala wa Rafiki Briquettes, Okoa Mazingira”
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Antony Mtaka ameipongeza STAMICO kwa kuja na suluhisho la utunzaji Mazingira kwa kubuni Mkaa Mbadala wa kupikia wakati ametembelea banda la STAMICO wakati wa Tamasha.
Ameikaribisha STAMICO katika mkoa wake ili iweze kujipatia malighafi ya makaa ili kuongeza nguvu katika uzalishaji.
Shirika la Madini linaendelea kutoa hamasa ya matumizi ya Mkaa Mbadala wa kupikia wa Rafiki Briquettes ili kuokoa mazingira, kwenye Tamasha la biashara liloanza tarehe 30 Desemba na kutarajiwa kufungwa Januari 13, 2023.