Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akihutubia wakati wa Kilele cha Matembezi maalum ya UVCCM ya kuadhimisha miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo tareheb10, January 2023 katika uwanja wa Kwacha, kijiji cha Paje mkoa wa Kusini Unguja
Mgeni Rasmi Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi mbalimbali meza Kuu wakishangilia wakati wa mapokezi ya matembezi ya vijana wa CCM yaliyofanyika kijiji Cha Paje mkoa wa Kusini Unguja kisiwani Zanzibar.
Mgeni Rasmi Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Akimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo wakati wa mapokezi ya matembezi ya vijana wa CCM yaliyofanyika kijiji Cha Paje mkoa wa Kusini Unguja kisiwani Zanzibar.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Shaka Hamdu Shaka akizungumza wakati wa mapokezi hayo.
………………………………….
Katibu mkuu wa Chama hicho Daniel Chongolo amewataka vijana wa CCM kuwa walinzi wa kukilinda Chama chao ili kiweze kutekeleza majukumu yake ya kuisimamia serikali Katika kuleta Maendeleo Kwa watanzania
Katibu Mkuu huyo ameyasema hayo wakati akihutubia Katika mapokezi ya matembezi ya vijana wa CCM yaliyofanyika kijiji Cha Paje mkoa wa Kusini Unguja kisiwani Zanzibar Jana Januari 10, 2023.
‘Ili kuendana na siasa za ushindani ni lazima tukumbushane na hasa kuwakumbusha vijana wa Chama cha mapinduzi (CCM) kuwa wana wajibu wa kuwa walinzi wa Chama hiki, kuwa watetesi wa Chama hiki, wajikite katika kutafuta taarifa sahihi kwa haraka na kuzielezea kwa wananchi ili yale yanayofanywa na serikali ya Chama cha mapinduzi yaonekane kwa Jamii,” Amesema Chongolo.
Aidha ameongeza kwamba kwa sasa chaguzi za viongozi wa ndani zimekwisha hivyo kwa sasa kilichobaki ni wanaccm kuwapa ushirikiano viongozi wapya ili waweze kufanya kazi zao kwa weledi kuzingatia itikadi na sera ya Chama hicho.