MUONEKANO wa Jengo Jipya la Diko na Soko la Samaki Malindi Wilaya ya Mjini Unguja lililofunguliwa leo 10-1-2023 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, ikiwa ni kuadhimisha sherehe za Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrissa Mustafa Kitwana alipowasili katika viwanja vya Diko na Soko la Samaki Malindi Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar kwa ajili ya kulifungua leo 10-1-2023.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi na Balozi wa Japan Nchini Tanzania Mhe.Yusushi Misawa, akiondoa pazia kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Ufunguzi wa Diko na Soko la Samaki Malindi Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar leo 10-1-2023 na (kushoto) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na Spaka wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zuberi Ali Maulid, ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi, wakitembelea jengo jipya la Diko na Soko la Samaki Malindi Wilaya ya Mjini Unguja,baada ya kulifungua ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Uchumi wa Buluu Zanzibar Mhe. Suleiman Masoud Makame, wakati akitembelea Diko na Soko la Samaki baada ya kulifungua leo 10-1-2023.(Picha na Ikulu)