Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Moses Nnauye leo Januari 9 2023 amazindua minara mitano ya Mawasiliano ya simu katika Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi na kuzungumza na wananchi Hafla ya Uzinduzi wa minara hiyo imefanyika katika mji wa Inyonga.
Na Chedaiwe Msuya. WHMTH
Serikali imesema inaendelea kuhimarisha huduma za mawasiliano nchini ili kuwaunganisha wananchi katika nyanja mbalimbali ikiwemo biashara na usalama.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) aliyasema hayo wakati wa ziara yake chuo kikuu cha sokoine cha kilimo,kijiji cha Kibaoni wilayani Mlele mkoa wa Katavi.
Alisema kuwa dunia ya sasa mawasiliano ndiyo kila kitu’’Mawasiliano ndiyo kila kitu kabisa na tunakoenda itafika mahali kama huna mawasiliano ni sawa na kutokuishi na ndiyo maana tumeanza kuzungumza kwamba huduma za mawasiliano ni haki za binadamu na ni sehemu ya vitu ambavyo vinakufanya uendelea kuishi,kwenye elimu ndiyo kabisa tena elimu ya utafiti kama za kwenu ndiyo kabisa usipounganishwa na mawasiliano kwa kweli unakua utimizi wajibu sawa’’alisema Nnauye.
Alisema katika chuo hicho wanakabiliwa na changamoto ya mawasiliano kutokana na kuwa na huduma kidogo ya TTCL.
“Nimekuja na injinia,mkurugenzi mwenyewe na TTCL ameseme hapa atafanya nini,amejipangaje sio tu kujipanga na lini tunamaliza hili jambo ili kuwadumia na wananchi wa eneo hili’’alisema Nnauye.
Kwa upande wa mtendaji mkuu wa mfuko wa mawasiliano kwa wote UCSAF Justina Mashiba alisema kuwa ni jukumu la UCSAF kupeleka huduma za mawasiliano vijijini kwa sababu makampuni ya simu pekee hayawezi.
“Kwa sababu baadhi ya maeneo vijijini hawapati faida Kwa hiyo serikali inaingiza fedha kidogo kama ruzuku ili watanzania wa maeneo mbalimbali waweze kupata huduma hiyo kwa hiyo mkurugenzi naomba unipatie maeneo sahihi vipo katika kata gani,lakini pia bado tunaendelea na miradi mbalimbali’’alisema Mashiba.
Awali mkuu wa chuo kikuu cha sokoine cha kilimo Zefania katani alisema wanakabiliwa na changamoto ya mawasiliano ya mitandao ya simu pamoja na masafa ya redio.