……………………
Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM )Wilayani Bagamoyo ,Abdul Sharifu amezuiwa na walinzi wa kiwanda cha Sea Salt kupita kuelekea Kitongoji cha Makupani ,Kijiji cha Saadani Kata ya Mkange Wilayani Bagamoyo alipokuwa akienda kusikiliza changamoto za wananchi ikiwemo kero kubwa ya kiwanda kushindwa kuwa na mahusiano mazuri na wananchi hao.
Kufuatia hali hiyo ,Sharif ameunda kamati ya watu kumi kwenda kwa mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kupeleka changamoto zinazowakabili wananchi wa Kitongoji hicho ambacho ni moja ya vitongoji vilivyo ndani ya Hifadhi ya Saadani.
Ameeleza kitendo hicho sio cha kistaarabu kwani wananchi hao wana haki ya kutembelewa na viongozi wao wa kisiasa na Serikali.
Hata hivyo aliuasa uongozi wa kiwanda cha chumvi cha Sea Salt kuwawajibisha walinzi wa kiwanda hicho ambao wanazuia misafara ya viongozi bila kujali wanakwamisha jitihada za Chama na Serikali kutoka maofisini kwenda kushughulikia kero za wananchi.
Sharifu alishangaa walinzi hao kuuzuia msafara wake kuingia kwenye kitongoji hicho na vitongoji vingine viwili vya Timba ,Kajanjo na kiwanda barabara ya kuingia vinatumia barabara moja ,geti moja la kuingilia lililowekwa na kiwanda.
Alieleza, moja ya changamoto ni wananchi kubanwa kuingia kwenda majumbani mwao wanapokuwa wametoka kwenda kufanya shughuli zao nje ya Vitongoji hivyo.
“Nimesikitishwa sana na walinzi hawa , maana kero kubwa niliyofikishiwa Ni wananchi kuzuiwa kupita katika geti hili kwenda majumbani kwao ,nimeshuhudia kwani msafara wangu nao umezuiwa “
“Vitongoji hivi viko kihalali na kisheria na vinatambuliwa na vina uongozi halali hivyo wana haki ya kutembelewa na viongozi wa Serikali na Chama ,wanahitaji kuongea na viongozi wao wakiwemo wa kisiasa na wataalamu,”alifafanua Sharifu.
“Nataka uongozi wa Kitongoji kuunda kamati ya watu kumi na kuandika barua ambayo itapeleka changamoto mlizonazo ili ziweze kutatuliwa mojawapo ni kuhusiana na masuala ya umiliki wa Ardhi ambapo linafanyiwa kazi na kamishna wa Ardhi wa mkoa,”alisema Sharifu.
Alibainisha kuwa viongozi mbalimbali walishafika kutatua baadhi ya changamoto lakini utekelezaji haujafanyika hivyo kikao na Mkuu wa Wilaya kitasaidia kujua nini cha kufanya kutatua changamoto zilizopo kisha serikali itatoa tamko.
Kwa upande wake Meneja Msaidizi wa kiwanda hicho ,James Gasore alieleza ,wazuia msafara huo kwakuwa ruhusa ya kuingia inatolewa na makao makuu ya ofisi yao.
Alieleza, hawajapata kibali cha kuruhusu ugeni huo kuingia kwenye eneo hilo hivyo hawana mamlaka ya kukubali waingie.
Akielezea moja ya changamoto walizonazo mkazi wa Kitongoji hicho Mohamed Salum alisema moja ya changamoto ni nyumba zao kubomolewa na kutakiwa kuondoka licha ya kuwa kihalali.
Aliiomba serikali itoe maelezo kama wao wako kihalali na kama hawako kihalali walipwe fidia ili wakaendelee na maisha yao sehemu nyingine.
Halima Jumanne alitaka uamuzi wa serikali juu ya hatma ya maisha yao,hawana amani, nyumba zao zinabomolewa wataishije na familia zao.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo Kasila Mgeni ,akizungumza kwa njia ya simu alieleza, suala la wakazi hao linafanyiwa kazi ambapo idara ya ardhi itatolea ufafanuzi.
Mgeni alisema ,serikali inajua changamoto zilizopo kwenye vitongoji hivyo na inafanyia kazi na wananchi wawe na utulivu na subira wakati masuala hayo yanashu