Dkt. Devotha Mandanda, Mwanasheria kutoka TASAC akifanya wasilisho la mapendekezo ya andiko la Sheria ya Utafutaji na Uokoaji.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Sekta ya Uchukuzi, Ndg. Shomari Omar Shomari (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pampja na baadhi ya wadau walioshiriki katika kikao cha kujadili andiko la mapendekezo ya Sheria ya Utafutaji na Uokoaji.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Sekta ya Uchukuzi, Zanzibar, Ndg. Shomari Omar Shomari (katikati), akizungumza na wadau wa usafiri kwa njia ya anga na maji kutoka SMZ na SMT wakati wa kujadili mapendekezo ya andiko la sheria ya Utafutaji na Uokoaji katika ukumbi wa ZURA, Zanzibar.
…………………………………
Wadau mbalimbali wa sekta ya usafiri kwa njia ya maji na anga wamekutaka kwa siku mbili kujadili kuhusu andiko la mapendekezo ya sheria ya utafutaji na uokoaji katika ukumbi wa ZURA uliopo Zanzibar tarehe 5 na 6 Januari, 2023.
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wakati wa kikao hicho Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Usafirishaji na Mawasiliano Zanzibar Ndg. Shomari Omar Shomari amesema sheria hii ni mihimu kwa pande zote mbili kwani usafiri wa anga na majini umeongezeka kwa kasi kubwa hivyo ni wakati muwafaka kukamilisha sheria ya utafutaji na uokoaji.
“Kutokana na majanga yanayotokea majini na angani basi hivyo matoke yanayotokea ni muongozo mzuri wa kufanya na kufuatia miongozo hiyo ya utafutaji wa anga na kubainika kuwepo na changamoto katika anga na bagarini, alisema Bw. Shomari.
Aliongeza kuwa anatambua juhudi za Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Sekta ya Uchukuzi kupitia katibu Mkuu kwa utamaduni wake wa kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na kuwezesha kufanyika kikao hiki muhimu Zanzibar ili kupata maoni ya pande zote mbili.
“Tunafahamu changamoto kwa sheria kama hizi zinazohusu Muungano kupata maoni mpaka kukamilisha utaratibu wa kutunga sheria, jambo hili alilolifanya ni muhimu sana pia inaonyesha ushirikiano wetu ulivyozidi kuimarika, aliongeza Bw. Shomari.
Pia alisema mbali na kuwa kumekuwa utungaji wa sheria hii unafuatia makubaliano na maelekezo yaliyotolewa na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO) na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Majini (IMO), hivyo kuwataka washiriki kuhakikisha sheria hiyo inasimamia masuala ya utafutaji na uokoaji kwa kuzingatia miongozo ya kimataifa.
Naye Mkurugenzi wa Idara ya Sera, Mipango na Utafiti kutoka Wizara ya Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi – Zanzibar, Bw. Makame Machano Haji amesema ni vyema kuwe na mfumo rasmi wa kisheria utakao toa nguvu kwa pande zote mbili kushirikiana kama Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pindi kunapotokea janga katika anga au majini.
“Suala hili linahitaji rasilimali fedha, watu na vifaa, nguvu ya upande mmjoja haiwezi kufamikisha kutatua tatizo hili hivyo tukiungana pamoja tunaweza kutatua tatizo kwa pamoja, alisema Bw.Machano.
Naye Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Sekta ya Uchukuzi Bw. Maseke Mabiki amesema jambo la muhimu ni wadau kuwa wazi kuelezea changamoto ili kuweza kuwa na sheria itakayosaidia pande zote mbili.
Wadau mbalimbali wa Sekta ya usafiri kwa njia ya anga na maji kutoka Serikali ya Muungano Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ambao ni Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi – Zanzibar, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA), Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TCAA) pamoja na Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar (KMKM) wamekutana kujadili andiko la Mapendekezo ya Sheria ya Utafutaji na Uokoaji.