Mtumwa wa Kanisa la Bwana Yesu kwa mataifa yote lililopo Tabata Kinyerezi Wilaya ya Ilala Philbert Paschal akizungumza na wanahabari Katika Ofisi za Kanisa Hilo jijini Dar es salaam
…………………………..
NA MUSSA KHALID
Viongozi wa Dini mbalimbali nchini pamoja na watanzania kwa ujumla wametakiwa kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ili aweze kuwatumikia wananchi na kukamilisha miradi mbalimbali ya Kimaendeleo kwa wakati.
Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es salaam na Mtumwa wa Kanisa la Bwana Yesu kwa mataifa yote lililopo Tabata Kinyerezi Wilaya ya Ilala Philbert Paschal ambapo amesema kuwa Mwaka huu Rais Samia atafanya mambo makubwa kwa wananchi wake jambo litakuwa ni faraja Kwa watanzania kwa ujumla.
Mtumwa Paschal akianza kueleza kuhusu mwaka 2022 amesema ulikuwa ni mwema na wenye changamoto mbalimbali zikiwemo za ukatili wa kijinsia na hiyo ikitokana na ukosefu wa maarifa.
“Sisi viongozi wa dini tunakazi Kubwa ya kuwaelimisha wauminui wetu namna kufanya kazi kwa ufanisi Ili waepukane kujihusisha katika vitendo vya ukatili” amesema Mtumwa Paschal
Akizungumzia mwaka huu wa 2023 Mtumwa Paschal amesema utakuwa mwema wenye maendeleo yatakayofanyika kwa spidi hivyo amewasihi Watanzania kutegemea makubwa kutoka kwa serikali inayoongozwa na Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluh Hassan
Amesema kuwa umoja Mshikamano na Upendo ndio nguzo kuu ya kuijenga Nchi hivyo amewakata watanzania kuendelea kumuombea Rais na taifa kwani Mwaka huu ni wamafanikio