WAZIRI MABULA ATOA SIKU 14 MAKAMPUNI YA UPIMAJI KUKWAMUA ZOEZI LA URASIMISHAJI VIWANJA
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula pamoja na viongozi wa Manispaa ya Temeke wakiwa katika picha ya pamoja na…
Latest updates on ministries, public service, parliament, policy decisions, and national administration.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula pamoja na viongozi wa Manispaa ya Temeke wakiwa katika picha ya pamoja na…
********************** Na Muhidin Amri, Ludewa WATUMISHI wa zahanati ya kijiji cha Nkomang’ombe Halmashauri ya wilaya Ludewa mkoani Njombe,wameondokana na kero ya kutembea umbali wa km 10 kila siku kwenda kuchota maji mto Mchuchuma kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwamo usafi na matumizi ya wagonjwa wanaofika kupata huduma ya matibabu. Sasa kero hiyo imekwisha baada ya wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa),kujenga mradi mkubwa wa maji katika kijiji cha hicho huku zahanati hiyo ikijengewa kituo kimoja cha kuchotea maji ambacho kimekuwa mkombozi kwa watumishi. Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo Sifael Mpolo alisema,kabla ya mradi huo walilazimika kwanza kwenda mtoni kutafuta maji kabla ya kuanza kuhudumia wagonjwa, hivyo kuathiri sana kazi utoaji huduma za matibabu kwa wananchi. Dkt Mpolo alisema,kufikishwa kwa huduma ya maji safi na salama katika kijiji hicho imesaidia watumishi kutekeleza majukumu yao kwa wakati kwa kuwa hawapaswi kwenda mtoni kuchota maji,badala yake wanatumia maji kutoka kwenye kituo kilichojengwa na Ruwasa. Aidha alisema,mradi wa maji ya bomba umesaidia sana kupungua kwa baadhi ya magonjwa ikiwamo matumbo,kuharisha na kichocho yaliyo sababishwa na matumizi ya maji yasio safi na salama kwa wananchi wa kijiji hicho. Dkt Mpolo,ameishukuru serikali kupitia Ruwasa kujenga mradi huo ambao umewezesha watumishi kupata muda wa kutosha,kufanya kazi kwa kujituma na weledi mkubwa ambapo amehaidi kutumia fursa hiyo kutoa huduma bora kwa wananchi. Meneja wa Ruwasa wilaya ya Ludewa Mhandisi Mlenge Nassibu alisema,mradi wa maji Nkomang’ombe umetekelezwa kwa gharama ya Sh.milioni 750 na unahudumia wananchi 3,500 wa vijiji viwili vya Kimelembe na Nkomang’ombe. Alisema,katika mradi huo wamejenga matenki mawili mapya na kukarabati tenki moja la zamani sambamba na ujenzi wa vituo 14 vya kuchotea maji katika maeneo mbalimbali ya vijiji hivyo na wananchi wameanza kutumia maji hayo kwa ajili ya shughuli mbalimbali. Mtendaji wa kata ya Nkomang’ombe Tumaini Ng’ande alisema,kupatikana kwa mradi huo kumemaliza migogoro mingi na ya mara kwa mara ya ndoa iliyosababishwa na wanawake kuchelewa kurudi nyumbani kutoka kutafuta maji kwa ajili ya matumizi ya familia zao. Aidha alieleza kuwa,mradi wa maji ya bomba umewasaidia wananchi wa kata hiyo kupata muda mwingi wa kufanya kazi za maendeleo ikiwamo ujenzi wa nyumba bora na kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii. Baadhi ya wanawake wa kijiji hicho,wameishukuru Serikali kupitia Ruwasa wilaya na mkoa wa Njombe kumaliza kero ya muda mrefu na kutumia muda mwingi kwenda kutafuta maji kwenye vyanzo vya asili na kumaliza vitendo vya ngono na migogoro kwenye ndoa zao. Ostazia Mgaya alisema,siku za nyuma walilazimika kuamka usiku kati ya saa 9 na saa 10 alfajiri kwenda kutafuta maji katika mto Mchuchuma unaopatikana umbali wa km 10 na kurudi saa 4 au 5 asubuhi. Alisema,kero hiyo ili sababisha kushindwa kushiriki kikamilifu kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo na wakati mwingine kukosa nafasi ya kuhudumia familia zao majumbani. Ester Haule, ameipongeza Ruwasa kukamilisha mradi huo ambao umeokoa ndoa za wanawake wengi wa kijiji hicho,hata hivyo ameiomba serikali kuendelea kuboresha baadhi ya huduma muhimu za kijamii ili kutoa fursa kwa wananchi kushiriki vyema shughuli mbalimbali za kiuchumi.
****************** Na Zillipa Joseph, Katavi Halmashauri ya Nsimbo ilyopo katika wilaya ya Mpanda mkoani Katavi imeanza mpango wa upandaji wa miti ya matunda katika…
Mwenyekiti wa Kamati ya Mawaziri wa Kisekta ambaye pia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki (Mb) akisoma maamuzi ya Baraza la…
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi akizungumza wakati hafla ya kufunga mafunzo ya…
Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Ilemela kimewataka viongozi wake kuwa mstari wa mbele katika kuchangia na kuhamasisha ujenzi wa ofisi za chama hicho kwa…
Na John Walter-Manyara Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Paulina Gekul amewataka wananchi kushiriki katika michezo ili kuimarisha afya zao na kuepuka maradhi…
Wizara ya Afya imekua mshindi wa kwanza miongoni mwa Wizara kumi ambazo zilichaguliwa na kushindanishwa kwa kutoa taarifa za Serikali kwa umma. Tuzo hiyo…
Na Alex Sonna MABINGWA Watetezi Yanga SC wameanza mzunguko wa pili kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Polisi Tanzania mchezo wa Ligi Kuu…