Katika kipindi cha mwezi Januari 2022 hadi hivi sasa jumla ya kesi za wizi wa mifugo zilizoripotiwa katika vituo mbalimbali vya Polisi hapa nchini ni 2934 ambapo jumla ya mifugo iliyoibiwa kipindi hicho ni 14530 yenye thamani ya Tsh. 6,719,024,600/= (bilioni sita milioni mia saba kumi na tisa elfu ishirini na nne mia sita).
Kufuata kesi hizo zilizoripotiwa Jeshi la Polisi lilianza uchunguzi wa kina na kufanikiwa kukamata watuhumiwa 1942 na kukamata jumla ya mifugo 4995 yenye thamani ya Tsh. 2,441,127,529/= (bilioni mbili milioni mia nne arobaini moja laki moja ishirini na saba elfu na mia tano ishirini na tisa) iliyokuwa imeibiwa maeneo mbalimbali hapa nchini.
Aidha katika kesi hizo zilizoripotiwa katika maeneo mbalimbali hapa Nchini na zilichunguzwa ambapo watuhumiwa 928 walifikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili. watuhumiwa hao walihusika katika matukio ya kuvunja Mazizi,wizi na unyang’anyi wa mifugo ikiwa malisho
Katika kuhakikisha tunalinda rasilmali za Nchi Jeshi la Polisi kupitia kikosi cha kuzuia na kupambana na wizi wa mifugo na migogoro ya wakulima na wafugaji Nchini limeendesha operesheni na kufanikiwa kukamata jumla ya mifugo elfukumi na tatu mia tano na mbili 13502. Kwa makosa ya kuingiza mifugo katika hifadhi za Taifa,mbuga ya Wanyama pori, Misitu na mapori tengefu.
Jumla ya mifugo iliyokamatwa katika operesheni hizo ilipigwa faini kiasi cha Tsh. 1,350,200,000/= Bilioni moja milioni mitatu hamsini na laki mbili kwa kosa la kuingiza mifugo hiyo katika maeneo ya hifadhi kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo.
Jeshi la Polisi kupitia kikosi cha kuzuia na kupambana na wizi wa mifugo Nchini litaendelea na operesheni Pamoja nakutoa elimu kwa wafugaji na wakulima Nchi nzima lengo likiwa ni kudhibiti vitendo vya kihalifu na wizi wa mifugo katika meneo mbali Tanzania bara na visiwani.
Natoa wito kwa wafugaji na wakulima wote Nchini kufuata matumizi bora ya ardhi ikiwa ni Pamoja nakutoingiza mifugo katika maeneo yaliyo hifadhiwa.Pia nitoe wito kwa wafugaji kujenga Mazizi imara lakini nitoe onyo kwa wafugaji kuto watumia Watoto wadogo katika kuangalia mifugo .
IMETOLEWA NA:
SIMON PASUA- ACP
KAMANDA WA POLISI
KIKOSI CHA KUZUIA WIZI
WA MIFUGO (STPU) NCHINI