WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na raia wa Uholanzi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume katika jengo la abiria la tatu ‘Terminal 3’ wakati alipofanya ziara ya kukagua utendaji kazi katika Uwanja huo, Zanzibar Disemba 29, 2022. Watatu kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Kaspar Mmuya, na wapili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Maduhu Kazi.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia) akimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA wa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege Zanzibar (ZAA), Mohammad Msoma akitoa maelezo ya maeneo mbalimbali ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume katika jengo la abiria la tatu ‘Terminal 3’ wakati alipofanya ziara ya kukagua utendaji kazi katika Uwanja huo, Zanzibar Disemba 29, 2022. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Kaspar Mmuya.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto) akimsikiliza Mfawidhi wa Uhamiaji Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Ali Juma Abdulkadir wakati alipofanya ziara ya kukagua utendaji kazi katika Uwanja huo katika jengo la abiria la tatu ‘Terminal 3’, Zanzibar Disemba 29, 2022. Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Hamza Hassan Juma.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto) akimsikiliza Maafisa wa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege Zanzibar (ZAA), waakitoa maelezo katika kitengo cha viza cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume katika jengo la abiria la tatu ‘Terminal 3’ wakati alipofanya ziara ya kukagua utendaji kazi katika Uwanja huo, Zanzibar Disemba 29, 2022. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu, Kaspar mmuya na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Maduhu Kazi.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Kaspar Mmuya, katika ukumbi wa watu mashuhuri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, jengo la abiria la tatu ‘Terminal 3’ wakati alipofanya ziara ya kukagua utendaji kazi katika Uwanja huo, Zanzibar
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na raia wa Uholanzi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume katika jengo la abiria la tatu ‘Terminal 3’ wakati alipofanya ziara ya kukagua utendaji kazi katika Uwanja huo, Zanzibar Disemba 29, 2022. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
………………………………….
Na Mwandishi Wetu, MoHA, Zanzibar
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kwa uwekezaji mkubwa uliofanyika wa ujenzi wa Jengo la abiria la tatu ‘Terminal 3’ katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.
Waziri Masauni ameyasema hayo mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza aliyoifanya usiku katika uwanja wa ndege huo akiwa ameambatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Hamza Hassan Juma, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara yake, Kamshina Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala pamoja na WaMaafisa mbalimbali wa Tanzania Bara na SMZ.
Masauni licha ya kuipongeza Serikali ya SMZ, pia ameipongeza Jeshi la Uhamiaji kwa jitihada kubwa za utendaji kazi unaofanywa katika Uwanja huo, kwa utoaji wa huduma zenye ufanisi na weledi na kuwataka waende sambamba na matakwa ya uwanja kwa kuendelea kutoa huduma kwa malengo ya serikali.
“Sijawahi kusafiri kwenda nje ya nchi kwa kupitia uwanja huu, kwa ziara hii ya leo ambayo nimeifanya jengo hili likiwa limekamilika, kwakweli huu uwanja una mvuto, hakika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inastahili pongezi kwa uwekezaji mkubwa uliofanyika wa ujenzi wa Jengo hili la ‘Terminal 3’ katika Uwanja huu wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume,” alisema Masauni.
Pia Waziri Masauni pia alizungumza na abiria wa mataifa mbalimbali walikuwa wanasubiria ndege ili waweze kurudi katika mataifa yao, pia aliangalia abiria wote wanapoingia nchini na jinsi huduma wanazopata kutoka kwa maafisa uhamiaji na pia alitembelea eneo la ukusanyaji wa mapato ya serikali katika Uwanja huo na kuwataka maafisa Uhamiaji kudhibiti mapato kwa kuendelea kuwa makini katika ukusanyaji wa mapato.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Hamza Hassan Juma amesema kuna changamoto zimeonekana ila anashukuru na kupongeza Mamlaka ya Uwanja wa Ndege Zanzibar (ZAA), kwa kuzifanyia ufumbuzi wa haraka ili kuweza kuendelea kuleta ufanisi sambamba na ushirikiano unaoendelea baina ya mamlaka hiyo na Jeshi la Uhamiaji katika utekelezaji wa majukumu Uwanjani hapo.
Naye Kamshina Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala amewahakikishia Watanzania kuwa Uhamiaji itaendelea kutoa huduma nzuri na maboresho ya kila siku ili kuhakikisha huduma za uhamiaji kwa wageni na wenyeji zinakuwa kwa kiwango bora cha kimataifa.
Waziri Masauni alifanya ziara hiyo baada ya kikao kazi cha siku moja kilichoshirikisha Uongozi wa Wizara yake na vyombo vyake vya usalama, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar.