Naibu Mwakilishi Mkazi wa UNICEF Tanzania Bw. Ousmane Niang akimkabidhi tuzo na cheti cha ushindi wa jumla kwa mwandishi Faraja Masinde Kutoka Mtanzania Digital baada ya kushinda tuzo ya jumla kuhusu habari za watoto (TEFCRA) kwa waandishi wa mitandao zilizoandaliwa na Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF na kufanyika leo Kwenye hoteli ya Peacock jijiniDar es Salaam leo Desemba 29,2022.
(PICHA NA JOHN BUKUKU)
………………………………
Waandishi 12 washinda Tuzo ya Umahiri wa Uandishi wa Habari za Watoto Tanzania
Wanahabari 12 kutoka katika vyombo mbalimbali wamepea Tuzo ya Umahiri katika Uandiahi wa Habari za Watoto nchini Tanzania.
Tuzo hizo zimetolewa na Shirika la Kuhudumia Watoto Tanzania (UNICEF) kwa kuahirikiana na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF).
Faraja Masinde kutoka Mtanzania Digital ndiye amepata tuzo ya jumla.
Walioshinda tuzo hizo ni Dk Tumaini Msowoya(Mwananchi – Shamba fmi), Marco Maduhu (Nipashe), Aidan Mhando (Chanel Ten), Faraja Masinde (Mtanzania) na Anord Kairembo (Radio Kwizera).
Wengine ni Vick Kimaro (Habari Leo), Jurieth Mkireri (Nipashe), Judith Ndibalema (Majira), Shua Ndereka (Mviwata Radio), Sabina Martine CHAI FM Rungwe Mkoani Mbeya , Anna Sombida (EATV) na Stansaus Lambet (Dar 24).
Mratibu wa tuzo hizo Neville Meena amesema huo ni mwendelezo wa kuhakikisha habari za watoto zinaendelea kuandikwa.
Makamu Mwenyekiti wa TEF, Bakari Machumu amewataka waandishi kuendelea kuandika habari za watoto.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Deodatus Balile amewata Wahariri na wanahabari kuingia kwenye vita dhidi ya Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971.
Naibu Mwakilishi Mkazi wa UNICEF Tanzania Bw. Ousmane Niang akimsikiliza Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri TEF Bw. Deodatus Balile katika tuzo za habari za watoto (TEFCRA)zilizoandaliwa na Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF na kufanyika leo Kwenye hoteli ya Peacock jijiniDar es Salaam leo Desemba 29,2022.
Mhariri wa Gazeti la Mwananchi Bw. Rashid Kejo akimkabidhi tuzo mwandishi Dkt. Tumaini Msowoya baada ya kushinda tuzo ya uandishi wa habari za watoto (TEFCRA)zilizoandaliwa na Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF na kufanyika leo Kwenye hoteli ya Peacock jijiniDar es Salaam leo Desemba 29,2022.
Afisa habari wa UNICEF Usia Nkoma akikabidhi tuo kwa mwandishi Aidan Mhando kutoka Channel Ten mara baada ya kushinda tuzo kwa upande wa luninga kuhusu habari za watoto (TEFCRA)zilizoandaliwa na Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF na kufanyika leo Kwenye hoteli ya Peacock jijiniDar es Salaam leo Desemba 29,2022.
Mhariri wa Gazeti la Raia Mwema Bw. Joseph Kulangwa akikabidhi tuzo kwa Mwandishi Vick Kimaro kutoka gazeti la Habari leo baada ya kushinda tuzo kuhusu habari za watoto (TEFCRA)zilizoandaliwa na Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF na kufanyika leo Kwenye hoteli ya Peacock jijiniDar es Salaam leo Desemba 29,2022.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri TEF Bw. Deodatus Balile akikabidhi tuzo kwa Mwandishi Marco Maduhu kutoka Gazeti la Nipashe Shinyanga baada ya kushinda katika tuzo za habari za watoto (TEFCRA)zilizoandaliwa na Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF na kufanyika leo Kwenye hoteli ya Peacock jijiniDar es Salaam leo Desemba 29,2022.
Mwanachama wa Jukwaa la Wahariri TEF Bw. Apornary Tairo akikabidhi tuzo kwa Mwandishi Stanslaus Lambert kutoka Dar 24 baada ya kushinda katika tuzo za habari za watoto (TEFCRA)zilizoandaliwa na Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF na kufanyika leo Kwenye hoteli ya Peacock jijiniDar es Salaam leo Desemba 29,2022.
Picha zikionesha baadhi ya waandishi wakiwa katika hafla hiyo.