Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Neville Meena amesema kuwa Mabadiliko yanayofanywa kwenye Sheria na sera ya mwaka 2023 lazima yataathiri Sera iliyopo sababu ya katiba iliyopo.
Akizungumza na blog ya fullshangwe meena alisema kuwa sheria yoyote ikitofautiana na sera,hulazimika kubadilishwa ili kukidhi haja ya sheria.
Meena alisema kuwa Kuna sheria ya habari ambayo inatarajiwa kupelekwa bungeni mwezi wa kwanza 2023 kwa ajili ya kufanyiwa marekebisho hivyo ni muhimu kuzingatia sera ya habari
Alisema kuwa katika mchakato wowote wa kutunga sheria, Sera huwa inatangulia kwanza na baadaye sheria inafuata.
“Kimsingi Mabadiliko yanayofanywa kwenye Sheria lazima yaathiri Sera iliyopo sababu haiwezi kukiuka Katiba na Sera “ amesema Meena.
Aidha alisema kuwa endepo kama Kuna mahali marekebisho yamefanywa kwenye Sheria na yakakinzana na sera lazima sera hiyo ibadilike ili iweze kuendana na Sheria iliyopo.
“Lakini pia kama kuna mahali marekebisho yamefanywa kwenye Sheria na yakakinzana na sera lazima sera ibadilike ili iweze kuendana” amesema Meena.
Hivi karibuni Waziri mwenye dhamana ya Habari Nape Nnauye akizungumza katika Kongamano la Kitaifa la Sekta ya inchini Jijini Dar es Salaam alizungumzia nia ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kuwasilisha Bungeni muswada wa marekebisho ya Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 ili kupitiwa upya na kufanyika marekebisho katika vifungu vyenye utata katika sheria hiyo