Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anaingia katika historia kubwa katika nchi hii kwa moyo wake thabiti wa kuipaisha Tanzania kiuchumi na kimiundombinu. Dkt. Samia Suluhu amekisikia kilio cha Mbunge wa Kisarawe Mhe. Dkt. Selemani Jafo, Mbunge wa Rufiji Mhe. Mohamedi Mchengelwa, na Kilio cha Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Alhaji Abbubakary Kunenge kwa kuiomba serikali kujenga barabara inayo unganisha Mikoa ya kusini ya Lindi na Mtwara na Mikoa ya Kaskazini ya Arusha, Kilimanjaro na Tanga kwa kupitia Mkoa wa Pwani bila ya kupitia Mkoa wa Dar es salaam ili kupunguza msongamano na kufupisha muda wa safari kwa wanaokwenda mikoa hiyo sambamba na kuimarusha uchumi na sekta ya utalii kupitia Hifadhi ya Taifa ya Nyerere na Bwawa la Nyerere.
Rais Dkt. Samia Suluhu amekisikia kilio cha muda mrefu cha Wana Pwani hivyo ameeleleza kujengwa kwa barabara ambayo itaanzia Utete – Mtemela – Vikumburu – Maneromango – Mzenga – Mlandizi – kuelekea Chalize. Hakika huu ni ukombozi mkubwa sana kwa Tanzania na wananchi wote wa Mkoa wa Pwani. Hakika Dua na Maombi ya wana -Pwani yapo kwa Rais wao Kipenzi Dkt. Samia Suluhu Hassani.
Hakika barabara hii itakuwa mbadala hata kwa wananchi wanao ingia jijini DSM kwani kwasasa Serikali inaendelea na ujenzi wa kiwango cha Lami kwa barabara ya Kisarawe Mjini kwenda Maneromango ambapo ujenzi huo unaendelea eneo la kijiji cha Sungwi hivyo mwananchi anayetoka Mikoa ya kusini anaweza kukwepa foleni ya maeneo ya Vikindu na Mbagala anaweza kupitia Utete – Kisarawe Mjiji – na kuingia katika Jiji la kibiashara la DSM ndani ya muda mfupi. Huu ni ukombozi mkubwa sana kwa Taifa letu.
Ni wazi barabara hii itaing’arisha Pwani kiuchumi na kuongeza mchango mkubwa kwa Pato la Taifa. Hongera sana Dkt. Salima Suluhu Hassani