Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Dkt. Noel Lwoga akimpatia mmoja wa wastaafu, Bw. Adrian Samagwa
Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Dkt. Noel Lwoga akimpatia Bibi Darila Yasini cheti cha utumishi
……..,………………..
Na Mwandishi wetu
Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Dkt Noel Lwoga amewapongeza wastaafu waliokuwa watumishi wa Taasisi hiyo kwa utumishi uliotukuka.
Akizungumza katika hafla ya kuwaaga wastaafu kutoka katika vituo vya Dar es Salaam na Arusha amewataka kuendelea kutoa mchango wao kwa Taasisi.
“Ninyi ni wataalamu katika maeneo mbalimbali hivyo muendelee kutoa ushauri juu ya kazi mbalimbali za Makumbusho” alisema Dkt Lwoga.
Amesema Taasisi yake itaendelea kuboresha mazingira ya kazi ya watumishi na kuhifadhi historia ya viongozi walitumika Makumbusho ya Taifa.
“Zawadi tulizotoa ni ishara na alama ya kuthamini mchango wenu katika Taasisi hii kwamba ulipita Makumbusho ya Taifa” alisema Dkt. Lwoga.
Mwakilishi wa wastaafu hao, Bw Adrian Samagwa ambaye alikuwa Mhasibu Mkuu ameushukuru uongozi wa Makumbusho ya Taifa kwa kuandaa hafla ya kuwaaga.
Ameuomba uongozi wa Makumbusho kutoa semina ya kujiandaa kustaafu kwa watumishi miaka mitano kabla ili wastaafu watarajiwa waweze kujiandaa.
Vile vile amewataka watumishi kufanyakazi kwa juhudi na maarifa na kwa uwajibikaji ili viongozi waweze kufikia malengo ya Taasisi