Mwenyekiti wa klabu ya Simba tawi la Mafinga Dickson Mtewele ambaye pia ni katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi akiongea na waandishi wa habari juu ya kununua gari kwa ajili ya wanachama wa timu hiyo.
Na Fredy Mgunda, Iringa.
WANACHAMA na mashabiki wa klabu ya Simba tawi la Mafinga mkoani Iringa wamepanga kununua gari kwa ajili ya kusafi kwenda kuishabikia timu hiyo.
Akizungumza wakati wa mkutano wa wanachama na mashabiki wa klabu ya Simba, mwenyekiti wa tawi la Mafinga Dikson mtevele alisema kuwa lengo la kufanya harambee ya kununua gari lao na kuacha tabia ya kukodi magari wakati wa Safari za kuifuta timu hiyo.
Mtevele alisema kuwa kununua kwa gari hilo kutasaidia kukuza uchumi wa tawi la Simba Mafinga kwa kulikodisha gari hilo katika shughuli mbalimbali wakati club ya Simba ikiwa haina ratiba ya mchezo wowote.
Alisema kuwa tawi la Mafinga linataka kujikuza kiuchumi na kuacha kuwa tabia ya kuchangishana na badala yake wataitumia coaster hiyo kufanya shughuli za kiuchumi na kusaidia wanachama na mashabiki wa Simba Mafinga kusafiri kuifuata timu mahali popote inapocheza.
Mtevele alisema kuwa katika harambee hiyo waliyoifanya wamefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi million 42 wakati gharama ya kununulia gari hilo ikiwa ni shilingi millioni 63.
Kwa upande wake mwanachama wa klabu ya Simba ambaye ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Mkoa wa Iringa, Daud Yassin alisema kuwa hatua waliyoifanya kutafuta pesa kwa ajili ya kununulia gari la kuwasafirisha wanachama na mashabiki wa Simba Kutachochea kuongeza idadi ya wanachama wa timu hiyo.
Yassin alisema kuwa kununulia kwa gari aina ya coaster kutasaidia kukuza uchumi wa wanachama wa tawi la Mafinga kwa kuwa watakuwa wameacha tabia ya kukodi gari kwa gharama kubwa hivyo watakuwa wanatumia gharama ndogo katika safari ya kwenda kuishangilia timu hiyo.
Alisema kuwa tawi hilo linawanachama zaidi ya mia ambao wanakadi za wanachama hai ambao wamekuwa wakilipia ada kila mwaka na michango mbalimbali ambayo inatakiwa kwa ajili ya maendeleo ya timu hiyo.