Wanafunzi walioshiriki mashindano hayo wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi hao
Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa atamizi ya DTBi- COSTECH Dkt Erasto Mlyuka akikabithi zawadi kwa washindi walioshinda katika mashindano hayo
Meneja mradi wa FSBL -DTBi ,Josephine Sepeku akizungumza na waandishi wa habari katika halfa hiyo jijini Arusha
…………………,…..
Julieth Laizer,Arusha.
Arusha.Jamii imetakiwa kuendeleza msingi wa vijana kuja na suluhu ya changamoto zilizopo katika nchi msingi ulioanzishwa na mradi wa Feature stem business leaders ikiwa ni pamoja na kubadilisha thamani ya elimu kuwa zao na huduma.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa atamizi ya DTBi- COSTECH Dkt Erasto Mlyuka katika mashindano ya kushindanisha shule saba za mkoa wa Arusha katika bunifu walizoziandaa zenye kutatua changamoto katika jamii kupitia mradi unaofanywa na taasisi ya Future STEM Business Leaders kwa kushirikiana na Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) na chuo kikuu Dar es salaam.
Dkt Mlyuka amesema kuwa mradi huo ulikuja baada ya institution ya taasisi ya Phizikia ya uingereza kuona Kuna changamoto katika Dunia kuwa wanafunzi wengi hawapendi masomo ya sayansi badala yake wanakimbilia kwenye masuala ya biashara na jammii haiwezi kufanya biashara bila kuwa na vitu vinavyotokana na masomo ya kisayansi.
“Leo hapa Arusha tumeona vijana wamekuja na suluhu ya changamoto tulizonazo kuna waliokuja na suluhu ya kimazingira na wengine mbolea sasa ni lazima mawazo kama haya tuendelee kuyalea ili yaje kutengeneza viwanda kwani chochote kinachofanya kazi leo chanzo chake kilikuwa ni wazo,” amesema Dkt Mlyuka.
Amefafanua kuwa wameonesha sampuli ya kifaa ambayo inaweza isitatue changamoto za hapa nchini tuu bali dunia nzima na wapo kwenye hatua ya kuhakikisha mfumo wa programu hiyo unaohusisha Mwalimu, Mwanafunzi na mtaalamu wa biashara ambaye yupo sokoni unaendelezwa nchi nzima.
“Niwapongeze wanafunzi wote, mmeanza safari ya ubunifu, hamtakaa mlale, ubunifu unahitaji kujitoa, kujali wengine na kujituma kwahiyo naamini zawadi mlizozipata na vyeti mlivyotunukiwa vitawakumbusha na kuwafanya mjione kumbe mnaweza,” Alisema.
Mkuu wa chuo cha ufundi Arusha (ATC) Dkt Musa Chacha amesema kuwa ni vema mradi huo umeona fizikia kama fursa kwani tatizo kubwa ni maarifa ambayo wanawapatia watoto ambayo wasipo tafsiri vizuri Mwanafunzi atapata A darasani lakina haina maana katika maisha yake.
Kwa upande wake Meneja wa mradi wa Future STEM Business Leaders (FSBL -DTBi) Josephine Sepeku amesema kuwa mradi huo unalenga kujenga na kutatua changamoto za biashara pamoja na sayansi ambapo wanafundisha wanafunzi wanaosoma sayansi kutumia sayansi za darasani kuzileta katika mfumo wa biashara na wanapitia hatua mbalimbali ikiwemo za kuwa wabunifu wa kutengeneza vitu vinavyotatua changamoto zilizopo katika jamii.
“Tunaposema vijana wajiajiri, tunaposena Tanzania ya viwanda tunaanzia hapa, tunawapatia mafunzo ili wao waweze kutengeneza na leo tumekuwa na shule saba ambazo zimeweza kushiriki, wanafunzi wakiwa ni 35 na wameweza kuja na bunifu mbalimbali na tumeweza kupata washindi watu,” amesema.
Ameongeza kuwa mshindi wa kwanza ni shule ya Arusha girls ambao wamekuja na kifaa cha utunzaji wa mazingira, ambapo inaleta usafi wa mazingira lakini pia kuleta biashara kutokana namkaa unaotoka katika kifaa hicho baada ya taka kuwekwa unaweza kutengenezewa matofali.
Amefafanua kuwa, mshindi wa pili ameweza kuleta suluhu ya changamoto tunazokutana nazo kama vile barabarani kwa kuja na mfumo unaoweza kupunguza ajali zinazotokea kutokana na kutokuelewa maeneo ya barabara au kutokufuata sheria pamoja na mshindi wa tatu ambaye ameweza kutengeneza mbolea isiyo na kemikali