Aliyeko kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Bravado group,Yasini Didas akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na huduma wanazotoa,kulia kwake ni Afisa masoko wa kampuni hiyo,Sharifa Abdallah.
………………..
Julieth Laizer, Arusha.
Arusha.Makampuni pamoja na taasisi mbalimbali zimetakiwa kutumia teknolojia za kisasa kutangaza biashara zao ili ziweze kujulikana ndani na nje ya nchi hususani katika kipindi hiki cha sayansi na teknolojia.
Hayo yamesemwa jijini Arusha na Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya masoko na uchapishaji ya Bravado Group ,Yasini Didas wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha.
Yasini amesema kuwa,umefika wakati sasa wa taasisi pamoja na makampuni mbalimbali kwenda kidigitali zaidi kwa kutangaza biashara zao kwa njia ya mtandao ili ziweze kujulikana ndani na nje ya nchi na kupata masoko zaidi.
Amesema kuwa, hivi sasa wafanyabiashara wengi wapo katika zama za ushindani mkubwa katika kufanya biashara sokoni ambapo kila mteja anatafuta namna ya kuweza kutangaza biashara ili ijulikane kimataifa kupitia kampuni hiyo.m
“Tunawasihi wateja watumie kampuni yetu kwa ajili ya kutangaza brand zao ili kwenda na kasi ya upelekaji habari na mahitaji ya huduma sokoni ambayo itaweza kuwafikia wateja wengi zaidi na kwa wakati mmoja.”amesema.
Amesema kuwa ,kampuni hiyo ilianza rasmi mwaka 2015 ambapo imekuwa ikitoa huduma mbalimbali ikiwemo kujitangaza biashara mbalimbali, masoko na huduma za uchapishaji.
Aidha amewataka wadau mbalimbali kutangaza biashara zao mtandaoni ili waweze kujulikana zaidi pamoja na kupata wateja ndani na nje ya nchi kwani kupitia kutangaza biashara hizo wataweza kuonekana kwa haraka shughuli zao wanazofanya badala ya kukaa kimya tu.