Afisa Mwandamizi kutoka ICPAC Collision Lore akitoa mada kwa wanahabari inayohusu namna ya kuandika taarifa za Hali ya Hewa katika warsha ambayo inafanyika kwa siku nne Nairobi Nchini Kenya.Mtaalamu na Mtengenezaji wa Tovuti ya IGAD/ICPAC Mr Erick Otenyo akiwaeleza waandishi wa habari kutoka Tanzania na Kenya Pamoja na wadau mbalimbali kuhusu matumizi sahihi ya mifumo kuhusu kuzipata taarifa zinazohusu Masuala ya Hali ya Hewa Ili kukabiliana na hatari katika warsha ambayo inafanyika kwa siku nne Nairobi Nchini Kenya.
Mshauri kutoka Ofisi ya Mamlaka ya Hewa Nchini Kenya -KMD Christine Mahonga akiwaeleza wanahabari Pamoja na wadau mbalimbali dhumuni la kufanya warsha hiyo ambayo inafanyika kwa siku nne Nchini Kenya.Afisa wa Program ya Uhakika wa Maji kutoka Taasisi ya Shahidi wa Maji Tanzania Tondelo Gungulundi akizungumzia namna sekta binafsi Jinsi gani inashiriki kwenye mnyororo wa masuala ya Hali ya hewa.
Baadhi ya wadau na wanahabari ambao wamehudhuria warsha hiyo ambayo inafanyika kwa siku nne Nchini Kenya
…………………………..
NA MUSSA KHALID
Wanahabari kutoka Nchini Tanzania Pamoja na Kenya wamejengewa uwezo wa kuandika na kutangaza taarifa mbalimbali zinazohusu Masuala ya Hali ya Hewa na Mabadiliko ya tabia Nchi ili waweze kuihabarisha jamii taarifa zisizokuwa na mkanganyiko katika maeneo yao.
Akizungumza wakati akifungua warsha ya siku nne kwa wanahabari wa Nchi ya Kenya na Tanzania wanaoandika taarifa zinazohusu Hali ya Hewa ambayo inafanyikia kwa siku nne Nairobi Nchini Kenya Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la ICPAC/CONFER Dr Mohamed Hassan amesema kuwa mafunzo hayo ni moja ya mfululizo wa shughuli ambazo wanazifanya kwa kuwajenga uwezo wa washirika wa ICPAC/CONFER katika Afrika Mashariki.
Amesema lengo lao hasa ni kuongeza uelewa na kuanzisha maelewano kati ya mamlaka za kitaifa za hali ya hewa, watunga sera, sekta binafsi na waandishi wa habari katika kutumia, kuwasiliana na kusambaza taarifa za hali ya hewa zinazotoka ICPAC.
“Ninawasihi wanahabari kuzingatia Mafunzo haya kwani yatawasaidia katika kuwajengea uwezo wa namna ya kuandika na kuripoti taarifa za Hali ya Hewa ambazo wanazipata kutoka katika Mamlaka husika katika nchi zao”amesema Dr Hassan
Kwa Upande wake Mshauri kutoka Ofisi ya Mamlaka ya Hewa Nchini Kenya -KMD Christine Mahonga amewataka wanahabari kuendelea kujifunza zaidi kwani itawasaidia kujiongezea ujuzi zaidi wa kuandika taarifa za Hali ya hewa.
Awali akizungumza kwa njia ya Mtandao Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini Tanzania Monica Mutoni ameeleza namna wanavyoshirikiana na vyombo vya habari Nchini Tanzania kuwa imesaidia Jamii kuwaamini kwa taarifa Mbalimbali wanazozitoa.
Aidha Monica amesema kuwa wamekuwa wakiwajengea uwezo wanahabari kupitia warsha mbalimbali Jambo ambalo limesaidia kwa kiasi kikubwa wapate uelewa wa kutosha wa kuandika na kutangaza habari zinazohusiana na masuala ya Hali ya Hewa.
Afisa Mwandamizi kutoka ICPAC Collision Lore akitoa mada Kwa wanahabari inayohusu namna ya kuandika taarifa ya Hali ya Hewa amesema wanaendeleza kampeni za pamoja za kukuza matumizi ya hali ya hewa na bidhaa za hali ya hewa kutoka kwa wadau wengine wa Kilimo na Usalama wa Chakula, Maji na Nishati.
“Pia dhamira yetu ni kuhakikisha wanahabari wanafahamu namna ya kupunguza Hatari za Maafa na Afya, kwa kushirikiana na watunga sera, waandishi wa habari, sekta binafsi na mamlaka ya hali ya hewa”amesema Like
Naye Afisa wa Program ya Uhakika wa Maji kutoka Taasisi ya Shahidi wa Maji Tanzania Tondelo Gungulundi amezungumzia namna sekta binafsi Jinsi gani inashiriki kwenye mnyororo wa masuala ya Hali ya hewa.