Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni, Ismail Seleman akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 2/12/ 2022 jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya utekelezaji kuanzia mwezi Julia hadi Septemba 2022.
………….
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kinondoni wamefanikiwa kufanya ufutiliaji wa utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo minne yenye thamani ya shillingi 1, 123,054,707.40.
Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 2/12/ 2022 jijini Dar es Salaam, wakati akitoa taarifa ya utekelezaji kuanzia mwezi Julia hadi Septemba 2022, Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni, Ismail Seleman, amesema kuwa miradi waliofatilia ni pamoja na ujenzi wa soko la chakula la Msasani Bonde la Mpunga ambapo mradi umeaza kutekeleza bila kuwepo kwa mkataba.
Seleman amesema kuwa mradi mwengine ni ujenzi wa jengo la dharura katika hospitali ya Wilaya ya Kinondoni ambapo kuna mapungufu ni nguzo na vyoo zilikuwa tofauti na zilivyoainishwa kwenye mkataba.
Pia kuna mradi wa ujenzi wa jengo la maabara na jengo la wazazi kituo cha Afya Amani ambapo eneo la mradi lipo katika mwinuko mkubwa na kupelekea kuongezeka kwa gharama za ujenzi.
Mradi mwengine ni uzalishaji wa fencing wire ambapo kuna ukiukwaji wa masharti ya urejeshwaji wa fedha za mikopo, ambapo mradi huo ulikopeshwa toka asilimilia 10 ya mapato ya ndani ya Halmshauri.
Seleman amebainisha kuwa pia wamepokea jumla ya taarifa 72 kati ya hizo taarifa zinazohusiana na vitendo vya rushwa zilikuwa 45 na zisizokuwa masuala ya rushwa ni 27.
Amesema kuwa taarifa 45 zilizohusu rushwa wamefungua majalada ya uchunguzi ambayo yanaendelea na uchunguzi wa kina na majalada manne yamekamilika na kwenda Ofisi ya Mashtaka.
Seleman ameeleza kuwa pia wamefungua kesi mpya tatu katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni na kufanya jumla ya kesi zinazoendelea mahakamani kuwa kesi 23, huku akibainisha kuwa kesi moja ilitolewa hukumu na Jamhuri ilipata ushindi.
“Tunaendelea kutoa huduma kwa wananchi wote kwa kutenga siku maalumu ya kusikiliza malalamiko na kero za wananchi kwa kuwafuata maeneo mbalimbali chini ya mapango wa TAKUKURU inayotembea” amesema Seleman.
Hata hivyo amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa TAKUKURU na kuepuka matapeli wanaoibuka na kuwapigia simu kwa kujifanya wao ni maafisa wa TAKUKURU, huku wakiwatapeli kwa kuwatisha kuwa wana tuhuma zao na kuwadai pesa ili wawasaidie kuzifuta hizo tuhuma.