Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akitoa leo hotuba mara baada ya kuwaapisha Mawakili wapya 384 katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaamMwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe Dkt.Eliezer Feleshi akitoa leo salama wakati wa halfa kuwaapisha Mawakili wapya 384 katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaamRais wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS) Prof. Edward Hoseah akitoa leo salama wakati wa halfa kuwaapisha Mawakili wapya 384 katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaamMawakili wapya 358 wakiapa mara baada ya kupokelewa na kuingizwa katika daftari la Mawakili katika Halfa iliyofanyika leo jijini Dar es salaamMawakili wapya 358 wakitoa heshima kwa Jaji Mkuu (hayupo katika picha ) mara baada ya kupokelewa na kuingizwa katika daftari la Mawakili katika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es salaamJaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof Ibrahim Hamis Juma (katikati) na jopo lake akipokea heshima kutoka kwa Mawakili wapya 358 walioapishwa leo Jijini Dar es salaamBaraza la Elimu ya Shule ya Sheria wakipokea heshima kutoka kwa Mawakili wapya 358 walioapishwa leo Jijini Dar es salaam.Picha na Mahakama ya Tanzania
………………………….
Na Tiganya Vincent-Mahakama ya Tanzania
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.Prof Ibrahim Hamis Juma amewataka Mawakili wapya 358 alioapitisha kutumia fursa ya maboresho ya ujenzi wa miundombinu ya Mahakama hapa nchini kufungua Ofisi zao karibu na Mahakama za Wilaya 20 zilizofunguliwa hivi karibuni ili waweze kutoa huduma yao huko.
Ametoa kauli hiyo leo katika Ukumbi wa Karimjee, Jijni Dar es salaam wakati wa Sherehe za 67 za kuwakubali na kuwaingiza kwenye daftari Mawakili wapya 358 na kufanya Tanzania kufikisha Mawakili 11,442 wa kujitegemea.
“Pelekeni huduma za Mawakili maeneo yote ya Tanzania, Mahakama ya Tanzania inaendelea na juhudi thabiti za kusogeza huduma ya utoaji haki karibu na wananchi,”alisema.
Mhe. Prof. Juma alisema tangu mwaka 2015 Mahakama ya Tanzania imejenga majengo ya kisasa kutoa huduma za Mahakama katika mikoa yote ya Tanzania.
Alisema majengo 20 ya Mahakama za Wilaya ambayo ameyazindua katika Wilaya za Mwanga , Same, Busega, Itilima, Butiama Rorya , Songwe , Gairo ,Mkinga , Mbogwe, Nyang’hwale, Kyera, Missenyi, Kaliua, Uvinza , Buhigwe, Kakonko, Tanganyika,Kilombero na Mvomero ni fursa kwao katika utoaji wa huduma za uwakili kwa wananchi wa maeneo hayo.
Mhe. Prof. Juma alisema baadhi ya wilaya hizo ni mpya na zina fursa za kutosha kwa Mawakili na zipo fursa nyingi za kiuchumi ambazo wanaweza kuzitumia ili kujipatia kipato na kujiendelea kimaisha.
Aliwashauri baada ya kuapishwa na kuingia katika daftari la Mawakili ni vema wakahama kutoka mijini na majiji ambako soko la uwakili lina ushindani mkubwa hasa kwa mawakili ambao bado hawajapata uzoefu wa kutosha na kwenda vijijini ambako kuna fursa ya kuwawezesha kujijengea uwezo wa kuendelea katika kazi yao.
Rais wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS) Prof. Edward Hoseah aliwataka Mawakili wapya kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili yaliyopo katika viapo vyao ili waweze kuepuka kujiingiza katika matatizo ya ukiukaji wa maadili ambayo yanaweza kuwasbabishia kukosa sifa ya kuendelea na utoaji wa huduma hiyo.
Alisema watakaobainiki kukiuka maadili watachukuliwa hatua kwa mujibu na taratibu na Sheria zinazolinda viapo vyao kama Maafisa wa Mahakama na kuna uwezekano wa kuondolewa katika daftari la Mawakili.
Prof. Hoseah aliongeza kuwa Chama cha Mawakili Tanganyika kinaendelea kupambana na vishoka ambao wamekuwa wakiendesha vitendo haramu na visivyo vya kimaadili ya kiutendaji kazi za uwakili na kuchafua taaluma hiyo muhimu kwa maendeleo ya Nchi.
Alisema vitendo hivyo vimekuwa vikisababisha kushuka kwa hadhi ya taaluma ya Uwakili na kusababisha kutoamini na Serikali na wadau mbalimbali katika jamii.
“Kuna baadhi ya watu wanaofanyika kazi za uwakili ingawa wao sio mawakili.watu hawa wamekuwa wakifanya kazi mbalimbali za kiuwakili kama vile kuandaa nyaraka , kuthibisha nyaraka , kushuduhia viapo. Wahalifu wa vitendo viovu ni watu wanaojifanya ni mawakili lakini sio mawakili, tunaendelea kupambana nao”alisisitiza.
Kwa upande wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe Dkt.Eliezer Feleshi alisema kumekuwepo na tabia ya baadhi ya Mawakili kujisahaulisha au kutoutendea haki wajibu wao wa kuisaidia Mahakama kufikia maamuzi ya haki kwa wakati.
Alisisitiza kuwa hiyo siyo tu kwamba si jambo jema lisilo na maadili, bali, linawaondolea baadhi hadhi ya kuwa Mafisa wa Mahakama wanapotekeleza wajibu wake kwa wateja wao.
Ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi,Alisema Mawakili ambao watashindwa kujiendelea ipo hatari kwao kujikuta wakinukuu Sheria ambayo imeshafanyiwa mabadiliko na haitumi tena.
“Kwa mfano, wakili anapoamua kufanya rejea kwenye uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufani, anapaswa kusoma uamuzi wote na kuuelewa na siyo kutumia aya moja ya uamuzi huo hivyo kuipotosha Mahakama pamoja na kwamba Mahakama nayo inalo jukumu la kuusoma ili kujiridhisha na usahihi wa hoja kwa mujibu wa uamuzi rejewa,” alisisitiza
Jumla ya Wakili wapya 358 wameapishwa na hivyo kufikisha idadi ya Mawakili 11,058 wa kujitegemea ambapo wanatoa huduma kwa wananchi mbalimbali hapa nchini