Naibu Katibu Mkuu akiwa amevaa kifaa cha kinachowezesha kutembelea Makumbusho kidigital alipotembelea Nyuma ya Utamaduni jijini Dar es SalaamNdani ya onesho la Mila Makumbusho na Nyumba ya UtamaduniNdani ya onesho la Mila Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Ndani ya onesho la Mila Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni
Ndani ya onesho la Mila Makumbusho na Nyumba ya UtamaduniNa
Naibu Katibu Mkuu, Bw. Juma Mkomi akiwa ameshikiria kata ya kifuu cha nazi ilyohifadhiwa katika Stoo ya Kijiji cha Makumbusho ambayo imejengwa kwa fedha za UVIKO19 alipotembelea makumbusho hiyo
Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Dkt Noel Lwoga akielezea umuhimu wa onesho la Kudumu la Mila linatengenezwa kwa fedha za UVIKo19 Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni jijini Dar es Salaam
……………………….
Na Mwandishi Wetu
Naibu Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Bw. Juma Mkomi ametembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Makumbusho ya Taifa katika vituo vya Nyumba ya Utamaduni na Kijiji cha Makumbusho na kufurahishwa na uhifadhi unaendelea katika vituo hivyo.
Bw. Mkomi akiambatana na Mratibu wa Miradi ya UVIKO 19, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt Consolata Kapinga alitembelea miradi inayotekelezwa katika Kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni kilichopokea TZS 303,000,000/- kwa ajili ya kuboresha stoo ya Histroria na ununuzi wa vifaa vya uhifadhi, kuboresha maabara na ununuzi wa vifaa vya maabara pamoja na madawa na kutengeneza maonesho mawili ya kudumi ya Mila na Biolojia.
Utekelezaji wa miradi hiyo unaendela vizuri ambapo karibu yote imekamilika kwa asilimia 100 isipokuwa miradi wa Bailojia ambao umekamilika kwa asilimia 85.
Aidha, Kijiji cha Makumbusho kilipokea jumla ya TZS 203,000,000/- kwa ajili ya kutekeleza miradi sita ikiwemo kujenga kaya tatu (Wasukuma Wazanaki na wahehe) kujenga stoo ya uhifadhi wa mikusanyo, kuboresha maabara na kununua vifaaa vya maabara, kujenga mfumo wa zimamoto, kujenga maombo ya nchi (Bahari ya Hindi na Ziwa Victoria) na mabango ya kujitangaza.
Utekelezaji wa miradi hiyo unaendelea vizuri ambapo karibia yote imekamika kwa asilimia 100 ambapo mradi wa ujenzi wa umbo la Bahari ya Hindi umekamilika kwa asili 90.
Naibu Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii ameipongeza Makumbusho ya Taifa kwa kazi ya uhifadhi wa teknolojia ya ujenzi wa nyumba za asili ambao unapotea katika vijiji vingi na kuitaka Makumbusho ya Taifa kuhakikisha kuwa miradi iliyosalia inakamilka haraka ili kazi ya uhifadhi iendelee na wananchi waweze kufaidika na uhifahdi huo
“Nawapongeza kwa utekelezaji wa miradi iliyokamilika kwa miradi iliyosalia mkamilishe haraka ili kazi iendelee” amesema Bw, Mkomi.
Amesema Lengo la Serikali katika miradi hiyo ni kuhakikisha uboreshaji wa uhifadhi unafanyika ili wananchi waendelee kutumia huduma hizo kwa maendeleo ya utalii nchini.
Naye Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa, Dkt. Noel Lwoga ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa Makumbusho ya Taifa ambazo imesaidia kuboresha Maonesho na miundombinu mingine ya uhifadhi katika vituo vya Makumbusho na Malikale.
“Tunashukuru kwa usimamizi mzuri wa Wizara yetu katika utekelezaji wa miradi hii maana imerahisisha kazi yetu ya uhifadhi,” amesema Dkt Lwoga