Kaimu Meneja Mkoa wa Kikodi Ilala Masau Clifford Malima akimkabidhi zawadi Mzee Joachim Michael kutoka kituo cha watu wenye Mahitaji Maalum cha Missionary Charity Nyumba ya amani na furaha katika muendelezo wa siku ya kipindi cha huduma na shukrani kwa mlipa kodi.
Kaimu Meneja Mkoa wa Kikodi Ilala Masau Clifford Malima akizungumza na waandishi wa habari akieleza dhamira ya kwenda kutoa zawadi katika kituo cha watu wenye Mahitaji Maalum cha Missionary Charity Nyumba ya amani na furaha
Mmoja ya wazee katika kutoa hicho Joachim Michael akitoa shukrani Kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania – TRA Mkoa wa Kodi Ilala baada ya kupatia msaada wa vitu Mbali kupatia vitu mbalimbali
Baadhi ya bidhaa ambazo zimetolewa katika kituo cha watu wenye Mahitaji Maalum cha Missionary Charity Nyumba ya amani na furaha katika muendelezo wa siku ya kipindi cha huduma na shukrani kwa mlipa kodi( picha na Mussa Khalid).
…………………………
NA MUSSA KHALID
Mamlaka ya Mapato Tanzania – TRA Mkoa wa Kodi Ilala imetoa zawadi mbalimbali na shukrani katika kituo cha watu wenye Mahitaji Maalum cha Missionary Charity Nyumba ya amani na furaha ili kusaidia shughuli zinazoendelea katika kituo hicho.
Akizungumza Leo jijini Dar es salaam katika ziara maalum ya Kutembelea katika kituo hicho Kaimu Meneja Mkoa wa Kikodi Ilala Masau Clifford Malima amesema huo ni muendelezo wa siku ya kipindi cha huduma na shukrani kwa mlipa kodi.
Amesema wao kama sehemu ya Jamii wamelazimika kwenda kutoa msaada katika kituo hicho kutokana na kuguswa kuonyesha mchango wao.
“Sisi kama wana Ilala tumeona kwa kipindi hiki tutumie muda huu kutoa shukrani kwa jamii yenye uhitaji ambapo tumekuja kuleta zawadi mbalimbali na tumezikabidhi kwenye uongozi kwani sisi kama Jamii tumeguswa sana”amesema Malima
Katika hatua nyingine Malima amesema Mkoa wa Kikodi Ilala wameendela kufanya shughuli zakukusanyaji wa mapato ambapo mpaka kufikia Mwezi Oktoba ufanisi wao umefikia Asilimia 104.5 katika lengo ambalo walipangiwa.
Amesema kutokana na Ushirikiano wanaoupata kutoka kwenye makundi mbalimbali ya walipakodi wanataraji kukusanya Trill 1.25 kwa mwaka huu wa Fedha.
Ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa makundi mbalimbali kuhakikisha wanalipa kodi ikiwa ni pamoja na kutumia matumizi ya EFD Ili kuendelea kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato.
Hata hivyo amewataka wananchi kuendelea kuonyesha ushirikiano kwa Mamlaka hiyo Ili waendelee kufanikisha ukusanyaji wa mapato Nchini na kusaidia serikali.
Kwa upande wake Mmoja ya wazee katika kutoa hicho Joachim Michael ameipongeza TRA Mkoa wa Kikodi Ilala Kwa kuonyesha kuguswa na kuwasaidia watu wenye uhitaji maalum.
Amesema kuwa yupo katika kituo Kwa Muda wa miaka Tisa hivyo ameiomba jamii kuonyesha moyo wa kuiga mfano wa TRA wa kuendelea kuisaidia Jamii misaada mbalimbali.