Msaidizi wa Askofu Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dean Lwiza (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi wa Mkutano wa 36 wa Kanisa hilo Bw. Daud Mnguruni wakati wakizungumzia na waandishi wa habari leo Novemba 24 Jijini Dar es Salaam.Msaidizi wa Askofu Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dean Lwiza akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 24 jijini Dar es Salaam kuhusu Mkutano Mkuu wa Kanisa hilo unaotarajia kufanyika Novemba 27 hadi 30, 2022 katika Ushirika wa Mbezi Beach.
…………………………
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani wanatarajia kufanya Mkutano Mkuu wa 36 utafanyika kwa siku nne kuanzia Novemba 27 hadi 30, 2022 katika Ushirika wa Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam.
Mkutano Mkuu wa mwaka huu utaongozwa neno kuu kutoka kwa Waefeso 4: 5 linasema “Bwana mmoja, imani moja, Ubatizo mmoja”.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 24, 2022 jijini Dar es Salaam, Msaidizi wa Askofu Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dean Lwiza, amesema kuwa mkutano huo unakwenda kujadili utekelezaji wa kazi mbalimbali zilizofanyika katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.
Msaidi wa Askofu Lwiza amesema kuwa pia wanakwenda kupanga mipango mengine ya miaka miwili ijayo kulingana mikakati ya Dayosisi.
“Tutajadili maendelo ya Dayosisi katika nyanja ya kuhubiri Injili na huduma za jamii ikiwemo afya, elimu, makundi maalum na mwenendo wa hali ya kiuchumi kwa ujumla” amesema Msaidizi wa Askofu Lwiza.
Ameeleza kuwa mkutano huo utaongozwa na Mwenyekiti ambaye pia ni Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani Dkt. Alex Malasusa.
Amefafanua kuwa katika Mkutano huo pia utakuwa na uchaguzi wa Wenyeviti wa halmshauri za idara na bodi za vituo.
Mkutano Mkuu wa 36 Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani unatarajia kuwa na wajumbe 424 kati yao ni wachungaji wote wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani.
Wajumbe wengine wa mkutano huo ni wawakilishi wa mabaraza ya wazee kutoka shirika 97 na mitaa 208 Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Maendelo Benki, Upendo Media, Chuo Kikuu Cha Tumaini Dar es Salaam pamoja na Taasisi zake.