Mkuu wa Kitengo cha Maliasili na mazingira Wilaya ya Mvomero Bi. Merry Massey akizungumza na waandishia wa habari kuhusu mradi wa Mkaa Endelevu ambao umekuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wa Wilaya hiyo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Maliasili na mazingira Wilaya ya Mvomero Bi. Merry Massey wakati akizungumza nao mradi wa Mkaa Endelevu ambao umekuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wa Wilaya hiyo wakati walipofanya ziara katika wilaya hiyo ili kukagua miradi hiyo ya utunziji wa misitu ya asiliya vijiji.
Mkuu wa Kitengo cha Maliasili na mazingira Wilaya ya Mvomero Bi. Merry Massey amesema kwamba mradi wa Mkaa Endelevu umekuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wa Wilaya hiyo kujua namna bora ya kuhifadhi misitu tofauti na vijiji ambavyo bado havijafikiwa na mradi lakini upande mwingine ukusanyaji wa mapato kupitia rasilimali za misitu umeongezeka na kuinua uchumi wa vijiji vilivyoko kweye mradi na wilaya hiyo
Bi. Merry Massey ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari walioko katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya Mkaa Enndelevu na utunzaji wa misitu ya asili inayotekelezwa na shirika la kuhifadhi Misitu ya asili Tanzania (TFCG) na Mtandao wa jamii wa usimamizi wa Misitu (MJUMITA).
Ameongeza kuwa kutokana na mradi huu wa Mkaa Endelevukuelekea ukingoni wilaya iko kwenye mpango wa kuandaa mkakati wa kuanzisha mfuko wa Halmashauri kupitia wadau wa wawekezaji ili kufanya mradi kuwa endelevu na kuenea kwenye vijiji vingine wilayani humo ambapo imetengwa kiasi cha fedha shilingi milioni 15 kwa ajili ya kuanzisha miradi hiyo katika baadhi ya vijiji tutakavyoanza navyo.
Kwa upande wake Afisa misitu Wilaya ya mvomero ndugu Edward Kimweri amesema Mradi wa mkaa endelevu ambao ulianzishwa kwenye Wilaya hiyo mwaka 2015 umeendelea kutekelezwa katika Wilaya ya mvomero mkoani morogoro ambapo mradi huo wa kuhifadhi misitu asili Tanzania TFCG wakishirikiana na MJUMITA pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero wameweza kutangaza misitu mitano(5) katika vijiji vipya ambayo imefikiwa na mradi huo, ambayo ni misitu ya vijiji vya Maraka, Usengere, Kipera, Kihondo na Msongosi huku vijiji vitatu vikiwa kwenye mchakato wa kuanzisha misitu mingine.
Edward ameongeza kwamba wananchi ya Wilaya hiyo walipewa elimu kuhusu namna bora ya kuhifadhi misitu na Wilaya iliandaa sheria ndogo ambazo zinasaidia kulinda misitu mpaka sasa tofauti na vijiji vingine ambavyo hakuna mradi huu.
Kupitia mradi Wilaya ya mvomero imepata manufaa mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuboresha hali ya misitu na jamii kuwa na uelewa mkubwa wa namna bora ya kuhifadhi misitu.
Mradi wa Usimamizi shirikishi wa Misitu ya jamiii(USMJ) ulikuwa unatekelezwa chini ya Mradi wa Kuhifadhi Misitu kwa kuwezesha biashara endelevu ya Misitu (CoForEST) kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la Uswisi (SDC).