Meneja mwandamizi anaesimamia sekta ya umma na taasisi kutoka Benki ya Equity Dkt.Danford Muyango (kushoto) akimkabidhi James Raphael kipeperushi baada ya kupewa elimu ya fedha kweye wiki ya Huduma za Fedha inayoendelea Jijini Mwanza
Meneja mwandamizi anaesimamia sekta ya umma na taasisi kutoka Benki ya Equity Dkt.Danford Muyango akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye banda lao
Wananchi wakiendelea kupewa elimu ya fedha
***********************
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Wananchi wametakiwa kuacha tabia ya kutunza pesa zao kwenye vibubu badala yake wapeleke kweye taasisi za fedha kwaajili ya usalama.
Rai hiyo imetolewa leo Jumatano Novemba 23,2022 na Meneja mwandamizi anaesimamia sekta ya umma na taasisi kutoka Benki ya Equity, Dkt.Danford Muyango, wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye Maadhimisho ya wiki ya Huduma za Fedha yanayoendelea katika viwanja vya Rock City Mall Jijini Mwanza.
Amesema wamekuwa wakitoa elimu kwa umma juu ya utunzaji fedha kwenye taasisi za kifedha hususani kwa watu ambao wako vijijini.
“Bado kunawatu wanaamini wakiweka fedha zao benki zinakuwa haziko Salama hivyo wanaamua kutunza kwenye majumba yao ndio maana tunaendelea kutoa elimu ili waweze kubadilika”, amesema Dkt.Muyango
Amesema Wananchi wanaohudhuria kwenye wiki ya Huduma za Fedha wasiishie kutembea bila kupata elimu ya fedha ambayo itawasaidia kuondokana na dhana potofu ya kutunza pesa kwenye nyumba zao.
Akizungumza mara baada ya kupatiwa elimu ya fedha James Raphael, amesema kutunza fedha nyumbani kunachangamoto nyingi zikiwemo za kuibiwa,kutumia fedha bila mpangilio hivyo ni vizuri zaidi kutunza fedha kwenye taasisi za fedha ambapo zitakuwa salama.